Wanafunzi walishwa kinyesi na mkojo chuo kikuu Msumbiji katika sherehe ya kuwakaribisha


Baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakiteswa katika chuo hichoHaki miliki ya pichaWHATSAPP
Image captionBaadhi ya wanafunzi waliokuwa wakiteswa katika chuo hicho
Sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wapya katika chuo kikuu cha Msumbiji imezua hisia kali baada ya picha kusambazwa katika mitandao ya kijamii zikioinyesha wanafunzi hao wanavyolazimishwa kunywa na kuoga mikojo na kinyesi.
Kulingana na mwandishi wa BBC Jose tembe mjini Moputoi, baadhi ya wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho cha kilimo, Misitu na uhandisi cha Unizambeze katikati ya mkoa wa Zambezi pia walinyolewa.
Kulingana na runinga ya kibinafsi ya STV , sherehe hiyo ilifanyika siku chache zilizopita.
Mwathiriwa mmoja , Artemiza Nhantumbo aliambia runinga hiyo kuhusu alivyoteswa.
''Waandalizi wa sherehe hiyo walitukata nywele zetu .Ilikuwa inatisha, ilikuwa haiwezi kuvumilika.Walitulazimisha kula mikojo na kinyesi . Tuliogeshwa na mikojo huku wakifuta pua zetu na vinyesi''.
Mwanafunzi mwengine Quiteria Jorge, alisema kuwa mwanafunzi ambaye alikuwa katika mwaka wa pili aliwatoa katika darasa lao ili kuwafanyia sherehe hiyo ya kukera.
''Walitukata nywele zetu kwa sababu wao wanahisi ni ndefu mno, lakini hatukuweza kufanya chochote, Nililia nikalia hadi nilipofika nyumbani''.
Kisa hicho hakikuwafurahisha wazazi wa wanafunzi hao ambao wamewataka wasimamizi wa chuo hicho kuwachukulia hatua hali wahusika.
Cardoso Miguel ambaye ni mkurugenzi wa elimu ya juu mkoani humo alisema kuwa uchunguzi unaendelea , ''kama tunavyoweza kuona picha katika mitandao ya kijamii ni wazi kwamba tabia hiyo haifai''
Kamati iliobuniwa itachunguza kiwango cha mateso hayo kwa kila mwanafunzi, huku wengine wakirudishwa nyumbani na wengine kufutiliwa mbali .
Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya sio rasmi lakini hufanyika sana katika vyuo vikuu nchini humo zikiandaliwa na wanafunzi waliopo katika mwaka wa pili.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA