Wastara atoboa siri kuachika mara tatu


Wastara
BAADA ya kuolewa mara tatu na ndoa hizo kuvunjika, staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ameibuka na kueleza siri za kuachika.
Akizungumza katika Tamasha la Single Mothers lililoandaliwa na msanii mwenzake, Faiza Ally na kufanyika katika Hoteli ya De Mag iliyopo Mwananyamala, Dar, Wastara alisema kuwa, siri kubwa ya ndoa zake kuvunjika ni kutokana na kukosekana kwa maelewano ndani ya nyumba na siyo kwamba huwa anapenda kuachika.
“Unajua kuna vitu ambavyo ningevikubali kuvifanya nilipokuwa ndani ya ndoa, ungekuta sasa hivi nimeshakufa hivyo kuolewa na kuachika siyo kupenda, bali nilishindwa kukubaliana na mambo ambayo nilikuwa ninalazimishwa kuyafanya,” alisema Wastara wakati akizungumza na wamama hao ambao wanawalea watoto bila baba zao.
Hata hivyo, aliwataka wamama hao kuwa na ujasiri wa kufanya kazi kwa bidii na wasinyong’onyee kwa sababu ya kuwa wanawalea watoto peke yao baada ya kuzalishwa na wanaume kuwakimbia au kuachika katika ndoa.
STORI:GLADNESS, Mallya
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA