Watu wanne wauawa na mshambuliaji aliyekuwa nusu uchi

 Mgahawa ulioshambuliaji kwa risasi na mtu aliyekuwa nusu uchi
Mtu aliyekuwa nusu uchi amewaua watu wanne katika mgahawa mmoja huko Nashville katika jimbo la Tennessee nchini Marekani.
Mtu huyo alianza kuwamiminia risasi watu waliokuwa katika hoteli hiyo na bunduki yake ambapo pamoja na kuwaua watu wawili,lakini pia amewajeruhi wengine wawili.
Polisi wanaendelea kumsaka mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Travis Reinking mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Illinois.
Don Aaron amesema kuwa Travis mwakajana alishikiliwa na Polisi pale alipojaribu kuingia katika eneo ambalo lipo karibu na Ikulu ya Marekani lenye kizuizini.
Hata hivyo James Shaw mmoja wa wateja katika mgahawa huo anapongezwa kwa ujasiri wake,aliouonyesha baada ya kumnyang'anya bunduki mshambuliaji huyo ambaye huenda bila hatua hiyo angeliua watu wengi Zaidi.
Lakini James mwenyewe alipopongezwa na kuishwa shujaa,amekanusha na kusema kwamba yeye alikuwa akijaribu kujiokoa tu na kwamba si shujaa.
Sheria ya umiliki silaha nchini Marekani bado inatoa mwanya wa kuzagaa kwa silaha hali ambayo imekuwa ikisababisha mashambulizi ya mara kwa mara ya silaha zinazomilikiwa na watu kwa urahisi.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA