ZIJUE KANUNI 5 ZA KILIMO CHA BIASHARA

DAR MVUA KUBWA!!
TAFAKARI! KILIMO CHA KIBIASHARA??
Wakati uku kwetu mvua inanyesha kwa wingi, ebu hapo ulipo jifunze kanuni za kilimo biashara na wataalamu wa mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA)
KANUNI 5 ZA KILIMO BIASHARA(SEHEMU YA KWANZA)
Kwa kifupi.
Uchaguzi Wa mbegu.
Kutoa katika kitalu hadi shambani.
Uwekaji mbolea.
Unyunyizaji dawa.
Kuweka maji katika mmea kwa wakati maalum.
Kuthibiti wadudu na magonjwa.
Kukomaa kwa matunda na mboga
Uvunaji mazao.
Utayarishaji wa mazao kwa mauzo ama kuhifadhi.
Napenda kuyasema hayo kwa sababu bidhaa au mazao yanayopatikana katika kilimo tunachofanya huuzwa katika masoko ya humu nchini na mengine soko la nje.
Ni muhimu kutaja hapa kwamba wanunuzi na walaji Wa mazao na bidhaa zinazotokana na mazao haya wanazidi kuwa waangalifu na huzingatia ubora wa mazao wanayopata kutoka kwa soko.
Mkulima anapaswa kuzingatia kanuni 5 zifuatazo hasa kabla hawajakurupuka na kuingia katika kilimo biashara.
NJIA YA KWANZA NI KUKUZA MIMEA.
Ni muhimu kwa mkulima kujiuliza je,? Katika msimu huu ni mmea gani ninastahili kupanda? Bila shaka mkulima anapaswa kufanya uamuzi kuhusu mmea au mimea atakayopanda na kukuza.
Ni vyema basi mkulima afanye makadirio ya gharama za mimea anayotarajia kupanda na kutambua faida kutokana na mimea hii mbalimbali itapatikana kwa kuandaa mpango kazi.
Akishatambua ni mimea gani anapanda na kukuza ni muhimu pia kuangalia mambo yafuatayo;
Aina gani au ni shina mama lipi litakalotumika wakati wa kupanda ubora wa mbegu kinga dhidi ya wadudu na magonjwa.
NJIA YA PILI NI WAKATI WA KUPANDA.
Kwa mkulima anayechukulia kilimo kama biashara, ni muhimu ajiulize je, ni wakati gani wa kupanda? Kwa wakulima wengi jawadu linalokuja kwa fikra zetu Mara moja ni wakati wa mvua. La hasha!! Wakati mzuri Wa kupanda unatambulika vyema tunapozingatia mambo fulani katika soko kama vile;
Ni wakati au muda gani mmea wako utakomaa?
Wakati uhitaji (demand) wa zao uko juu pale ambapo bidhaa huwa adimu sokoni.
Wakati bei ya mazao ni nzuri kwa mkulima.
Wakati utoaji( supply) wa zao uko chini kabisa.
Ni muhimu kwa mkulima kuwa na muongozo wa upandaji mazao yake na vizuri zaidi akatushirikisha wataalamu pia wakati huo huo awe ameshadadisi uhitaji wa mazao sokoni.
TATU NI MAHALI PA KUKUZA
Mimea huleta mazao mazuri na mengi hasa unapopandwa eneo ambalo kitaalamu udongo wake utalandana na zao hilo. Hivyo mkulima aidha aupime udongo wake au aulizie historia ya eneo hilo analotengemea kwenda kupanda mimea yake. Kuchunguza eneo kutasaidia kupata taarifa pia ya wadudu wasumbufu na wanyama pia. Lakini pia kuyajua magonjwa hatarishi kwenye eneo husika. Inasikitisha sana kuona mkulima anaotesha mbegu zake kisha akija anakuta wanyama kama panya wameshazitafutana. Hii inatokea sana na hivyo kumpotezea mkulima malengo yake na humletea gharama. Haya yote hutokea kama mkulima hatoifanya kazi kanuni ya kuchagua mahali sahihi pa kukuzia mmea wake.
NNE UPANDAJI NA UKUZAJI.
Katika kilimo cha biashara ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo.
.utayarishaji shamba; shamba ni sharti zitayarishe ipasavyo kwa kuchimbua kikamilifu, kuondoa manyasi, magugu hatari na kuinua mchanga kimo cha sm.5 kwa kuboresha mazao na wingi wake, ni muhimu atumie mbinu zilizo na gharama ya chini lakini apate faida kubwa. Basi mkulima inapaswa awe na utaalamu wa kilimo biashara.
NA TANO NI WATEJA.
Wateja wa kisasa hujali sana ubora wa mazao na afya zao. Ni muhimu kwa mkulima kutambua mahitaji na matakwa ya wateja wake kabla ya kupanda na kutunza mimea yoyote.
Mwisho.
Hizo ndizo kanuni tano za kufanikiwa katika kilimo biashara.
Imeletwa kwenu na
Ally Said (0678970256)
Email.kihoro48@gmail.com
Mtaalamu wa kilimo biashara na masoko MKIKITA
MKIKITA
Back to the Land
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

DK MAGUFULI AZISAMBARATISHA NGOME ZA MBOWE, NDESAMBURO NA NASSARI

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

WAKIANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA, MBOZI