*DAR ES SALAAM KUMEKUCHA, RAIS MAGUFULI ASHUSHA NEEMA.*


Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam wameendelea *kula Matunda* ya serikali ya awamu ya tano baada ya *Rais Dr. John Magufuli* kutoa zaidi *Shilingi Billion 250* kwaajili ya utekelezaji wa *Miradi Mkakati* ya *kuziwezesha Halmashauri* za jiji hilo *kujiendesha zenyewe* ili kupunguza *utegemezi* wa fedha kutoka Serikali kuu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* amesema miongoni mwa *miradi* itakayotekelezwa ni pamoja na *ujenzi wa kituo cha kisasa cha Mabasi ya Mikoani Mbezi Luis* kitakachogharimu zaidi ya shilingi *Billion 50* ambacho ujenzi wake utaanza *Mwezi June* na kuchukuwa *miezi 18* kukamilika.
*RC Makonda* amesema jengo hilo litakuwa na *gorofa tano* ambapo kituo hicho cha kisasa kitakuwa na uwezo wa kuchukuwa *Mabasi 200* na Maegesho *magari 300* (Underground parking) ambapo ndani kituo kutakuwa na huduma zote muhimu ikiwemo *Hotel, Hostel, Shopping Mall,Maduka, Migahawa, sehemu za mapumziko, Kituo cha Polisi, Bustani, Bank, Vyoo* vya kisasa pamoja na *Ofisi za kampuni za Magari.*
Aidha *RC Makonda* amesema miradi mingine ni Ujenzi wa *Soko la kisasa Kisutu* litakalogharimu shilingi *Billion 16*, Kituo cha Mabasi *Chamanzi Mkondogwa*, Ujenzi wa *Machinjio ya kisasa Vingunguti* yenye thamani ya *Billion 8.5* itakayokuwa na uwezo wa kuchinja *Ng'ombe 1,000* kwa siku hali itakayoondoa *uagizwaji wa Nyama Nje ya nchi* kwaajili ya kuuzwa kwenye *Hotel na Supermarket* ambapo kukamikika kwa mradi huu utawezesha *wazawa kupata soko la nyama la uhakika*, Ujenzi wa *Soko la Mburahati Billion Billion 2.7 kituo cha Daladala Tuangoma, Soko la Kibada Billion 14* pamoja na *miradi mingine mingi* ikiwemo *Fukwe za Coco, Ujenzi wa Shopping Mall* na miradi mingine lukuki inayofanywa na *Rais Magufuli* kwenye Mkoa wa Dar es salaam.
*RC Makonda* amemshukuru *Rais Magufuli* kwa kwa dhamira njema ya kusaidia *kutatua kero za wananchi* ambapo amewasihi wananchi wa Dar es salaam kukaa *mkao wa kula* kwa kuchangamkia *fursa za ajira* zitakazotolewa kwenye *miradi* hiyo.
*HUU NI UPENDO WA DHATI WA RAIS MAGUFULI KWA WANANCHI WAKE.*
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA