Kanye West asema Wamarekani Waafrika 'walipendelea' kuwa watumwa


Msanii wa muziki wa rap nchini Marekani Kanye West,Haki miliki ya pichaPA
Image captionKanye West hivi majuzi alirekodi wimbo akitetea kumuunga mkono Donald Trump
Msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West amesema kuwa utumwa wa Wamarekani Waafrika uliofanyika zaidi ya miaka 100 iliopita lilikuwa chaguo lao.
'Unaposikia kwamba utumwa ulifanyika kwa zaidi ya miaka 400.. miaka 400? ni kama walipendelea hilo kufanyika', alisema katika tovuti ya burudani ya TMZ.
Nyota huyo hivi karibuni aligonga vichwa vya habari kwa kumuunga mkono rais Donald Trump.
Watu weusi walilazimishwa kutoka Afrika na kuelekea Marekani katika karne za 17, 18 na 19 na kuuzwa kama watumwa.
Presentational white space
West baadaye alituma ujumbe wa Twitter na kusema kwamba hakueleweka vyema na kwamba alizungumza kuhusu miaka 400 kwa sababu 'fikra zetu' haziwezi kufungwa kwa miaka mingine 400.
Katika mahojiano na TMZ West alisema hivi sasa tunachagua kufanywa watumwa swala lililozua hisia kali kutoka kwa mfanyikazi mmoja mweusi katika kampuni hiyo.
Bwana Lathan alisema kuwa matamshi ya msanii huyo yalionekana kutolewa bila kufikiria.
"Una haki ya kuamini chochote unachotaka , lakini ujue kuna ukweli katika dunia ya sasa na athari zake kwa kila kitu ulichosema', aliongezea huku nyota huyo akisimama na kujikuna kidevu.
"Lazima tukabiliane na ukandamizaji uliotokana na mika 400 ya utumwa ambayo ulisema kuwa watu wetu walipendelea, bwana Lathan aliendelea akiongezea kwamba nimeshangazwa na ndugu yangu nimeumizwa kwa wewe kusema kitu ambacho sio cha kweli.
Katika mahojiano hayo ya TMZ West amemtaja bwana Trump kuwa rafiki yake na kusema kuwa rais huyo ni miongoni mwa watu wake anaowapenda sana.
Matamshi yake yalizua hisia kali katika mitandao ya kijamii huku watumiaji wa mtandao wa twitter wakisema kuwa msanii huyo anafaa kusoma upya vitabu vya historia.
Presentational white space
Inajiri siku chache tu baada ya West kutoa wimbo ukimtetea rais Trump ambaye amesisitiza kuwa anapigania Wamarekani.
Wimbo huo uliozua utata Ye vs p The People ulizua hisia kali miongoni mwa wasanii akiwemo Snoop Dogg ambaye alionekana kukasirishwa na maneno ya wimbo huo.
"Like a gang truce, the first Blood to shake the Crip's hand," West raps, akitaja makubaliano kati ya magenge mawili ya mjini Los Angeles.
Mpwa wa Snoop Dogg msanii Daz Dillinger baadaye alichapisha ujumbe wa video akiwataka wanachama wa genge la Crip kumkabili Kanye iwapo watakutana naye mjini California.
Kanda hiyo ya video inachunguzwa na polisi kulingana na ripoti.
West amezua hisia kali kutokana na hatua yake ya kumuunga mkono Trump na wahafidhina kama vile Scott Adams na Candace Owens, ambaye amezungumza dhidi ya vuguvugu la Black Lives Matter.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA