Madrid yatinga fainali ya tatu mfululizo UEFA


Karim Benzema (kulia) alifunga magoli yote mawili
Image captionKarim Benzema (kulia) alifunga magoli yote mawili
Mabingwa wa Ulaya kwa upande wa vilabu Real Madrid imefanikiwa kutinga hatua ya fainali muchuano ya Ligi ya mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuindosha Bayern Munich ya Ujerumani kwa jumla ya magoli 4-3.
Wakiwa na faida ya magoli 2-1 ugenini, Real Madrid ilihitaji sare ya aina yoyote ili kuweza kutinga fainali ya michuano hii mikubwa kwa upande wa vilabu barani Ulaya.
Joshua Kimmich alianza kufunga kwa mapema kipindi cha kwanza kabla ya Karim Benzema kuisawazishia Madrid baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Marcelo.
Ulikuwa mchuano uliovutia wengi
Image captionUlikuwa mchuano uliovutia wengi
Makosa ya mlinda mlango wa Bayern Sven Ulreich yaliizawadia Madrid goli la pili lililopachikwa na Benzema kabla ya James Rodriguez kusawazisha.
Bayern walikua na nafasi ya kuondoka na ushindi lakini mikwaju ya Corentin Tolisso na Thomas Muller iliokolewa vyema na mlinda mlango Keylor Navas ambaye alikuwa katika kiwango kizuri.
Real itakumbana na Liverpool ama Roma katika fainali itakayopigwa mjini Kiev, Ukraine May 26.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.