Mwanamke ahukumiwa kifo kwa kumuua mumewe aliyembaka Sudan


Wanawake nchini Sudan wamekuwa wakiishi katika jamii zinazodhibitiwa na wanaumeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWanawake nchini Sudan wamekuwa wakiishi katika jamii zinazodhibitiwa na wanaume
Mahakama moja nchini Sudan imemhukumu kifo mwanamke mwenye umri wa miaka 19 kwa kumuua mumewe aliyembaka.
Jaji wa mahakama hiyo iliopo Omdurman alithibitisha hukumu hiyo ya kifo baada ya familia ya mumewe mwanamke huyo kukataa kufidiwa kifedha.
Wakati alipokuwa na umri wa miaka 16 , Nourra Hussein alilazimishwa kuingia katika ndoa na familia yake.
Hakuwa na raha hatua iliomlazimu kutoroka na kujificha katika nyumba ya shangazi yake.
Lakini miaka mitatu baadaye , anasema kuwa alidanganywa arudi nyumbani na familia yake ambayo ilimrudisha tena kwa mumewe.
Baada ya siku sita mumewe aliwaita binamu zake ambao walimzuia chini na mumewe akambaka. Wakati alipojaribu kumbaka tena siku iliofuata Nourra alimdunga kisu mumewe hadi akafariki.
Alitoroka na kurudi kwa wazazi wake ambao walimwasilisha kwa maafisa wa polisi.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake Jaji huyo aliipatia familia ya mumewe chaguo la kumsamehe Nourra lakini ikachagua auwawe.
Kesi yake imevutia hisia kali katika mitandao ya kijamii ambapo kampeni kwa jina #JusticeforNoura imekuwa ikisambazwa katika mtandao wa Twitter.
Mawakili wake wamewasilisha ombi la hukumu ndogo ya mauaji.
Wakati huoho kundi la wanaharakati wa kupigania haki za kibinaadamu la Equality Now limesema kuwa litamwandikia rais Omar al-Bashir kumuomba amuonee huruma.
Mahakama inoyosimamiwa na Sheria ya kiislamu ilimuhukumu bi Hussein kwa mauji yaliopangwa mwezi uliopitwa na siku ya Alhamisi ikatoa hukumu ya kumnyonga kulingana na chmbo cha habari cha reuters
Mawakili wake wana siku 15 kukata rufaa.
Chini ya sharia za kiislamu familia ya mume inaweza kutaka ifidiwe kwa kulipwa fedha au iombe kifo, kulingana na mwanaharakati Badr Eldin Salah kutoka kwa vuguvugu la vijana ambaye alikuwa katika mahakama hiyo.
''Walichagua kifo na sasa hukumu imetolewa''.
  • Je mashirika ya haki za kibinaadamu yanasema nini?
Yasmeen Hassan wa Equality Now, mojawapo ya makundi yanayotaka hukumu hiyo kubadilishwa , aliambia BBC kwamba hukumu hiyo haikumshangaza.
''Sudan ni taifa ambalo wanawake wanaishi chini ya usimamizi wa wanaume na kanuni za kijinsia hufuatwa'' , alisema.
Ni taifa ambalo wasichana huruhusiwa kuolewa wakiwa na umri wa miaka 10.Kwa Noura ni msichana ambaye alitaka elimu na alitaka kufanikiwa na amekwama katika hali hiyo na sasa ni mwasiriwa wa utawala wa eneo hilo.
Shirika la Amnesty International limesema kuwa hukumu ya mwanamke ya kifo ambaye alikuwa akijitetea inaangazia uzembe wa serikali kukabiliana na ndoa za watoto , ndoa za lazima na ubakaji katika ndoa.
''Utawala wa Sudan ni lazima ukabiliane na hukumu hiyo isiokuwa ya haki na kuhakikisha kuwa Nourra anapewa hukumu ya haki'', ilisema AI .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.