Raia wa Ujerumani atekwa Somalia


Wapiganaji nchini SomaliaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWapiganaji nchini Somalia
Mfanyakazi wa Shirika la Kimataifa la msalaba mwekundu raia wa Ujerumani ametekwa nyara katika mji mkuu wa Somalia.
Habari zinasema watu wasiofahamika waliokuwa wamebeba silaha, walimteka ndani ya eneo la ofisi hizo mjini Mogadishu na kumtoa nje kwa kutumia mlango wa nyuma, ili kuweza kuwakwepa walinzi waliokuwa katika lango kubwa la mbele.
Msemaji wa Shirika la Kimataifa la Msalaba mwekundu amesema wana wasiwasi mkubwa na usalama wa mfanya kazi mwenzao.
Amesema muuguzi huyo aliyetekwa alikuwa akifanya kazi kila siku kuokoa maisha ya baadhi ya Wasomali wenye hali mbaya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*