TAASISI YA UHUSIANO WA UMMA TANZANIA (PRST) KUADHIMISHA WIKI YA MAWASILIANO AFRIKA MEI 25, 2018 JIJINI DAR
Taasisi
ya Uhusiano wa Umma Tanzania, (PRST) inatarajia kufanya maadhimisho ya
wiki ya Mawasiliano Afrika, iliyoanza tokea Mei 21 na kilele chake
kinatarajiwa kuwa Mei 25, 2018 na Tanzania watafanyia kwenye Ofisi ndogo
ya Bunge iliyopo Posta Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Chama hicho hapa
Tanzania, Ndege Makura, amesema ili kufanikisha siku hiyo wameamua
kuweka mezani maada inayoendana na agenda kuu ya siku hiyo Kitataifa ya
Uchumi wa pamoja barani Afrika, wao wamekuja na Tanzania ya Viwanda.
Amesema
takribani ya Mataifa yote yamekua katika kusherekea siku hiyo ya
mawasiliano ambapo jumla ya miji 60 Barani Afrika wanasherekea ikiwemo
na Tanzania. Aidha amesema kuwa katika kongamano hilo, yapo malengo
bainishwa Kimataifa huku Bara la Afrika wakijadili uchumi wa pamoja
lakini kwa Tanzania watajadili suala la mchango wa Maafisa Uhusiano wa
Umma ni kwa jinsi gani wanaweza kuchangia kuleta maendeleo ya uchumi
hususani katika suala zima la kutangaza sera ya Tanzania ya Viwanda.
"Hii
ni siku muhimu kwetu watu wa Uhusiano wa Umma , kwani tutajadili vitu
vingi vinavyotokana na Sera za maendeleo ya Taifa, wapo watu wengi
hawaelewi nini maana ya Viwanda, dhumuni lake na njia za kufikia ndoto
hiyo ya Rais wetu, hata Bungeni tumeona Wabunge wakikinzana kuhusu
viwanda, tunaleta mjadala huu ili kujadili kwa kina na wataalamu wetu ,
Wizara ya Viwanda, Afisa uhusiano wa umma kutoka Serikalini na Taasisi
binafsi, waandishi wa habari, ili kusaidia ndoto ya Taifa letu kufikia
malengo ya Tanzania ya viwanda ifikapo 2025" amesema Makura.
Nae
Rais wa PRST, Loth Makuza amesema kuwa umefika wakati wa kwenda
kumkwamua afisa habari wa taasisi au shirika binafsi ili aweze
kujitambua na kutambua malengo ya serikali yake kwa kujua umuhimu wa
kazi yake. "Kuna Maofisa Habari wengi hawajitambui hasa kwa kuwa nyuma
kabisa kwa vile wengine hawajui hata malengo ya serikali au mashirika
yao, matokeo yake wao huishia kuandika taarifa za kuambiwa badala ya
kuwa wao wawe miongoni mwa watu wanaoweza kuzitokea ufafanuzi zaidi na
kwa kina," amesema Makuza.
Ameongeza
kuwa changamoto nyingi za kutokukamilika kwa Sera mbali mbali za
maendeleo hapa nchini kutofikia lengo ni kutokana na kutoshirikishwa
hivyo watu wamekuwa wakichelewa kupata taarifa na kujua kwa kina juu ya
utungwaji wa Sera hizo. , Amewaomba wadau wajitokeze kwa wingi ili
kuchangia mambo ya msingi yanayohusu maendeleo ya Taifa letu pamoja na
uchumi wa pamoja katika Bara letu la Afrika.
Barani
Afrika Makao Makuu ya Taasisi ya Uhusiano wa Umma yapo mjini Lagos
Nigeria na duniani hapo uingereza Taasisi ya Uhusiano wa Umma Tanzania,
(PRST) ilizinduliwa rasmi mwaka jana Novemba 2, mwaka 2017, Jijini Dar
es Salaam kwenye ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania, huku ikitimiza zaidi
ya wanachama 200, ambapo miongoni mwao wametokea kwenye Taasisi binafsi
walizo ajiriwa na wengine kutoka Vyuoni.
Katibu
wa Taasisi ya Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) Ndege Makura,
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Mei 22, 2018
jijini Dar es Salaam wakati akielezea maadhimisho ya wiki ya Mawasiliano
Afrika inayotarajiwa kufanyika katika Ofisi ndogo ya Bunge iliyopo
Posta. Pembeni yake ni Rais wa PRST, Loth Makuza.
Rais
wa Taasisi ya Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST), Loth Makuza akitoa
msisitizo kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono katika
maadhimisho ya wiki ya Mawasiliano Afrika inayotarajiwa kufanyika katika
Ofisi ndogo ya Bunge iliyopo Posta. Kushoto ni Katibu wa PRST, Ndege
Makura. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Na Cathbert
Kajuna - Kajunason/MMG.
Comments