Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 03.05.2018


Anthony Martial
Image captionAnthony Martial
Jose Mourinho yuko tayari kumchezesha Anthony Martial katika safu ya kati ya mashambulizi msimu ujao iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atakubali kusalia Manchester United. (Mail)
Manchester United imempatia kipau mbele beki wa kushoto wa Juventus na Brazil Alex Sandro, 27, kuchukua mahala pake beki wa kushoto wa Uingereza Luke Shaw, 22, msimu ujao. (Manchester Evening News)
Manchester United imempatia kipau mbele beki wa kushoto wa Juventus na Brazil Alex Sandro, 27,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionManchester United imempatia kipau mbele beki wa kushoto wa Juventus na Brazil Alex Sandro, 27,
Manchester City inapima uzito wa kumsajili mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Jamaican Leon Bailey, 20. (Goal)
Claude Puel huenda akapoteza kazi yake kama mkufunzi wa Leicester iwapo hatamaliza vizuri ligi hiyo(Talksport)
Fernando Torres
Image captionFernando Torres
Klabu ya ligi ya Major League nchini Marekani DC United ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Uhispania Fernando Torres, 34, au mshambuliaji wa Boca Juniors na Argentina Carlos Tevez, 34. (Goal)
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Marouane Fellaini, 30, anaamini kwamba Manchester United ilifanya makosa kwa kukataa kumuongezea kandarasi yake mara moja na badala yake kumwacha katika hali nzuri ya kuhamia klabu nynegine. (Sport Voetbal Magazine. via Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Ubelgiji Marouane Fellaini, 30,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
West Brom iko tayari kuanza mazungumzo na mkufunzi wa Brentford Dean Smith na naibu kocha wa Leicester Michael huku wakianza kumsaka meneja mpya.. (Mail)
Rafael Benitez anataka kuwepo kwa makubaliano kuhusu hatma yake na Newcastle kuhusu bajeti yake ya uhamisho na uwezo huku klabu hiyo ikijaribu ikimfunga kwa kumpatia kandarasi mpya ya muda mrefu. (Mirror)
Rafael Benitez
Image captionRafael Benitez
Mshambuliaji wa Uhispania Gerard Deulofeu, 24, hatarajii kurudi katika klabu iliomkuza Barcelona mwisho wa msimu huu akisema kuwa Watford bado inamtaka kusalia msimu ujao.. (Cadena SER - in Spanish)
Chelsea inataka kulipwa kitita cha £10m ili kumuuuza kiungo wa kati wa Uholanzi Marco van Ginkel, 25, ambaye ameshiriki katika ligi ya Premia kwa dakika 11 pekee (Football.London)
Kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 24Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 24, anasema kuwa hafikirii kuhusu hatma yake na kwa sasa anajaribu kuisaidia timu hiyo kutoshushwa daraja kutoka katika ligi ya Premia msimu ujao (Reuters)
Burnley inapanga kuwasajili beki wa Bristol City Joe Bryan, 24 kwa kitita cha £6m. (Mirror)
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MBUNGE MOLLEL AITAKIA NAMAINGO MAFANIKIO MEMA 2019

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA