Unai Emery: Ninataka Arsenal wawe klabu bora zaidi duniani



Meneja mpya wa Arsenal Unai Emery amesema anataka klabu hiyo kuwa miongoni mwa klabu bora zaidi Ulaya kwa mara nyingine, na hata bora duniani.
Alisema hayo alipohutubiwa wanahabari kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa kuwa mrithi wa Arsene Wenger.
Mkufunzi huyo wa miaka 46 aliwasilishwa rasmi kwa mashabiki na wanahabari Jumatano kabla yake, akiandamana na afisa mkuu mtendaji Ivan Gazidis kuhutubia waandishi wa habari waliokuwa wamefika kwa wingi.
Alisema: "Ufanisi msimu ujao utakuwa bado tunaukuza, lakini kwa jinsi gani? Kwa kupigania kila taji.
"Hilo limo ndani ya historia ya Arsenal na yangu mwenyewe."
Arsenal walishindwa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2017 na hawatashiriki michuano hiyo msimu wa 2018-2019. Awali, walikuwa wamefuzu kila mwaka tangu 1998.
Mhispania huyo
Gazidis alifichua kwamba Mhispania huyo alikuwa kwenye orodha ya wakufunzi wanane ambao walikuwa wamewekwa kwenye mizani kumtafuta mtu wa kumrithi Wenger, lakini yeye ndiye aliyekuwa naatafutwa zaidi.
"Wote wanane walishiriki mahojiano ya kina na hakuna hata mmoja aliyejiondoa kwenye mchakato huo," Gazidis alisema.
Aliongeza kwamba kazi hiyo ni moja ya zinazotutia zaidi katika ulimwengu wa soka.
"Tuna bahati sana kumpata mtu tuliyemtafuta tangu awali.
"Mahojiano yetu ya kwanza tuliyafanya mnamo 25 Aprili na ya mwisho tuliyafanya 15 Mei. pendekezo la mwisho kwa bodi lilitolewa likiambatana na barua ya kurasa 100 yenye maelezo ya kina.
"wanachama wote wa bodi walifurahia uamuzi wetu."
Gazidis wanasema meneja huyo wa zamani wa Valencia, Sevilla na Paris St-Germain aliwapendeza sana waliokuwa wanafanya mahojiano hayo kutokanana jinsi "alivyokuwa amejiandaa".
"Alifanya vyema saa na alikuwa amejiandaa tena kwa ujuzi wake kuhusu Arsenal na utathmini wa wachezaji wetu, uwezo wao na jinsi wanavyoweza kuboreshwa.
"Jambo lililowatenganisha na wengine ni jinsi tulivyohusiana vyema na hisia za soka zilivyojitokeza chumbani.
"Ana hisia fulani na moyo wa ushindani na ana moyo anapenda soka. Hizi pamoja na azma yake ya ushindi ndivyo vilivyotufanya kuamini kwamba anaifaa Arsenal."
Emery aliwaambia wanahabari kwamba alisafiri kwenda Atlanta akiandamana na Gazidis, mkuu wa uajiri wa wafanyakazi Sven Mislintat na mkuu wa uhusiano wa soka wa klabu hiyo Raul Sanllehi ili kukutana na mwenyehisa mkuu Stan Kroenke na familia yake.
"Tunataka kufanyia kazi klabu hii kwa pamoja," aliongeza.
"Naijua azma yangu na kujitolea kwangu na najua ninavyotaka kukua pamoja na Arsenal.
Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Emery alihariri maelezo yake kwenye Twitter baada ya uteuzi wake, kuonesha majukumu yake mapya
"Mazungumzo yote nimekuwa nayo na klabu hii yanaonesha tuna ndoto moja kwa klabu hii."
Arsenal walimaliza nafasi ya sita Ligi ya Premia msimu uliopita, nafasi yao ya chini tangu walipomaliza nafasi ya 12 msimu wa 1994-95.
Mashabiki wamekuwa wakilalamikia uwezo wa wachezaji wa klabu hiyo kwa sasa.
Alipoulizwa iwapo atahitaji kuajiri wachezaji zaidi majira yajayo ya joto, Emery alisema: "Ninaamini tunaweza kukua na wachezaji tulio nao.
"Lengo ni kufanya kazi kwa pamoja na wachezaji hawa wenye vipaji.
"Ni muhimu sana kwa klabu hii, baada ya kukaa miaka miwili nje ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, kufanya kazi kuwa klabu bora zaidi Ligi ya Premia na hata duniani."
Alimsifu sana pia Wenger ambaye ameongoza klabu hiyo kwa miaka 22.
"Kwa wakufunzi wote duniani, yeye ni wa kurejelewa. Tulijifunza, nilijifunza mambo yote kuhusu soka kutoka kwake.
"Ni changamoto kwangu, lakini pia nimefanya miradi mingine, miradi mikubwa. kwangu, najivunia kuwa hapa na kufanya kazi baada ya Arsene Wenger."
Emery ametimiza nini?
Emery, 46, amejiunga na Gunners baada ya kuondoka PSG ambapo aliwaongoza kushinda ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1.
Mhispania huyo pia alishinda vikombe vya ligi mara nne akiwa na miamba hao wa Ufaransa.
Awali alikuwa meneja wa Sevilla ambapo aliwasaidia kushinda Europa League mara tatu mtawalia.
Mameneja walivyoshinda Kombe la UEFA/Europa League
Meneja Mara YMiaka Klabu
Giovanni Trapattoni 3 1977, 1991, 1993 Inter Milan, Juventus
Unai Emery 3 2014, 2015, 2016 Sevilla
Luis Molowny 2 1985, 1986 Real Madrid
Juande Ramos 2 2006, 2007 Sevilla
Rafa Benitez 2 2004, 2013 Valencia, Chelsea
Jose Mourinho 2 2003, 2017 FC Porto, Manchester United
Diego Simeone 2 2012, 2018 Atletico Madrid

Mada zinazohusiana

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*