UTAFITI: Kutokula matunda kunavyochelewesha kushika mimba


Bila shaka umewahi kusikia tafiti nyingi pamoja na wataalamu wa masuala ya afya wakieleza madhara ya ulaji wa vyakula vya mafuta mengi ikiwa ni pamoja na kuongezeka uzito, magonjwa ya shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na mengineyo.
Utafiti mpya ambao umefanywa na wanasayansi wa Chuo kikuu cha Adelaide, Australia wamegundua kuwa ulaji wa vyakula vya mafuta mengi na sukari bila kula matunda mengi, huweza kusababisha tatizo la kuchelewa kupata ujauzito kwa wanawake.
Utafiti huu ambao umefanyika kwa wanawake nchini Australia, New Zealand, Ireland naUingereza wameeleza kuwa walibaini kuwa wanawake wanaotumia matunda mara tatu kwa mwezi, wanachukua kiwango cha nusu mwezi kwa wastani kushika mimba.
Hii ni tofauti na wanawake ambao hula matunda mara tatu au zaidi kwa siku ambao hushika mimba haraka zaidi.
Utafiri umeeleza kuwa wanawake wasiokula matunda kwa wingi wana hatari ya 12% ya kutokuwa na uwezo wa kushika mimba katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja ukilinganisha na 16% ya wanaokula chakula chenye mafuta mengi, mara nne au zaidi kwa wiki.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI