Utafiti: Malazi ya Sokwewatu ni masafi kuliko ya binaadamu


Malazi ya Sokwe mtu ni masafi kuliko ya binaadam, wanasayansi wamebaini. Viumbe hawa hujenga malazi kwa kutumia matawi na majani ya miti ambapo hulala.
Malazi ya sokwe mtu ni mfano kwa mwanadamu kijana ambaye anaweza kuona vigumu kufuata
Mwanafunzi wa Marekani wa shahada ya Uzamivu Megan Thoemmes, aliyeongoza jopo kukusanya sampuli za uchafu kutoka kwenye Sokwe watu 41 katika bonde la Issa nchini Tanzania: ''Tunajua kuwa makazi ya binaadamu yana aina mbalimbali ya viumbe.
''Mfano, takriban asilimia 35 ya vijidudu kwenye vitanda vya binaadamu vinatoka kwenye miili yetu wenyewe, ikiwemo, kinyesi, kinywani na vijidudu vya kwenye ngozi
''Tulitaka kujua ni kwa namna gani hali hii inaweza kufananishwa na Sokwe hawa,ambao huandaa vitanda vyao kila siku.
Sokwe mzee zaidi kwenye hifadhi afariki Marekani
Kumbe sokwe sio wapenzi wa muziki
Ikilinganishwa na vitanda vya binaadamu, sehemu za kulala ya sokwe zilikuwa na aina mbalimbali za wadudu, matokeo ambayo hayakutarjiwa katika misitu ya kitropiki
Haki miliki ya picha Lwiro Primates and Anthony Caere
Hata hivyo,uwezekano ni mdogo sana kwa sokwemtu kupata ''uchafu'' kinyesi, kinywa au bakteria kwenye ngozi.
''Hatukuona vijidudu kwenye malazi ya Sokwe mtu, jambo lililoshangaza kidogo'', alieleza Bi Thoemmes kutoka Chuo cha North Carolina .
Walishangazwa na walichokigundua walipojaribu kusafisha malazi ya hao chimpanzee kuondosha viroboto na chawa waliokuwepo.
Watafiti wanasema vitanda vya Sokwe watu ni visafi zaidi kuliko vya binaadamu, ingawa viumbe hawa hutumia zaidi ya nusu siku kitandani.
Wanasayansi wamegundua kuwa malazi ya Sokwewatu nchini Tanzania yana kiasi kidogo cha kinyesi na bakteria kuliko magodoro ya binaadamu majumbani, kwa sababu viumbe hawa huhama malazi kila usiku.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

FAHAMU DALILI KUU ZA AWALI ZA MIMBA KUSHIKA

MAFUNZO YA UONGEZAJI THAMANI VIAZI LISHE YAFANA SUGECO

JIONEE WAREMBO KUMI WA NGUVU AFRIKA MASHARIKI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

ANGALIA PICHA WADADA HAWA WALIVYOPIGWA

PADRI AUGUSTINO RAMADHANI AONGOZA IBADA YA KUMBUKUMBU YA MKE WA PROFESA SHABA DAR

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!