Wavulana
waliozaliwa na baba ambao wana matatizo ya kutoweza kuwafanya wanawake
kutunga mimba huenda wakawa na kasoro sawa na hivyo ikilinganishwa na
wenzao waliotungwa kwa njiya ya kaiwaida.
Hii ni kwa mujibu wa
utafiti mpya wa afya ya uzazi. Watafiti wamesema kwamba wavulana ambao
baba zao hushindwa kuwafanya wanawake kutunga mimba watarithi matatizo
hayo ya kizazi. Wanasayansi hutumia njiya ya kutoa manii ya mwanamme aliye na uchache wake na kisha kuyadunga kwenye mayai ya mwanammke ili kutunga mimba. Mbinu hii ilianzishwa miaka ya tisini.
Watafiti walifawafanyia uchunguzi wanaume waliozaliwa kwa kwa njiya ya kutoa manii ya baba zao na kudunga kwenye mayai ya mwanammke na kugundua kwamba walikua na kasoro sawa na baba zao. Kwa mujibu wa mtafiti mkuu Profesa Andre Van Steirteghem amesema hii ndiyo mara ya kwanza imebainishwa kwamba watoto wa kiume wanaweza kurithi kasoro za uzazi zilizo na baba zao.
Comments