WANAKIJIJI WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWAPATIA FEDHA ZA UVIKO 19 KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA SEKA SEKONDARI+video


 

Seka Sekondari ilifunguliwa mwaka jana (Julai 2021) na sasa ina WANAFUNZI wa Kidato cha Kwanza na Pili.


Sekondari hii ni ya PILI ya Kata ya NYAMRANDIRIRA ambayo ujenzi wake ulianza kwa MICHANGO kutoka kwa:


(i) Wanavijiji: fedha taslimu na nguvukazi

(ii) Mbunge wa Jimbo: fedha zake binafsi

(iii) Mfuko wa Jimbo: fedha za Serikali

(iv) Baadhi ya Wazaliwa wa Kata ya Nyamrandirira


*DAFTARI lenye orodha ya MICHANGO limetunzwa na Serikali ya Kijiji cha Seka.


KATA hii ya Nyamrandirira yenye VIJIJI 5 (Chumwi, Kaboni, Kasoma Mikuyu na Seka) kwa sasa inazo SEKONDARI MBILI (2) ambazo ni:


*Seka Sekondari

*Kasoma Sekondari yenye "HIGH SCHOOL" ya Serikali.


Tafadhali wasikilize, WANAVIJIJI na VIONGOZI wao wakimshukuru Rais wetu, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia FEDHA za kujenga vyumba vipya 4 vya Madarasa kwenye Sekondari yao mpya.


"CLIP" imeambatanishwa hapa  - tafadhali isikilize.


Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Musoma Vijijini

www.musomavijijini.or.tz



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA