DKT.KIKWETE AWAASA WAZAZI PWANI KUTHAMINI ELIMU KWA WATOTO




Na Mwamvua Mwinyi ,Pwani
Rais Mstaafu Awamu ya nne, dkt.Jakaya Kikwete amewaasa wazazi na walezi Mkoani Pwani, kushikilia na kuthamini elimu kwa watoto kwani ndio urithi wao wa baadae.
Alitoa rai hiyo , wakati Taasisi ya kifedha ya Stanbic ,ilipokabidhi vyumba vya madarasa Kumi na madawati 100 kwa taasisi ya Watoto Wetu Tanzania, inayojihusisha na kutoa elimu kwa watoto wenye Mazingira magumu na hatarishi huko Mazizi ,Msata Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani.
Alisema ,Elimu Ni ufunguo wa Maisha , endapo wazazi wakwere,wazigua,wazaramo,wadoe watabakia kulia  kuwa Ni wachiwa, maskini basi tutapoteza muelekeo wa watoto.
Alieleza,  baadhi ya Mila zilegezwe ili watoto wapende shule huku tukiendelea kudumisha tamaduni zetu.
Hata hivyo, Jakaya amesema upo namba kumi kwa ufaulu Sekondari na shule za msingi ,amewaomba watoke huko na kupanda tano bora hadi kufika wa kwanza.
Amemuelekeza mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge kukaa na walimu wakuu wa Sekondari ili kujitafakari taaluma ya mkoa na kuangalia sababu zinazosababisha kutofanya vizuri zaidi kwenye Sekondari na shule za msingi .
Nae Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge,aliwapongeza Stanbic Bank kwa moyo wao wa kutoa na kuthamini watoto wenye Mazingira magumu.
Kunenge alielezea, mkoa kwasasa upo katika kumi bora kwa ufaulu,wanakwenda vizuri na wamejipanga kuendelea kuinua taaluma na kuboresha Mazingira  kwenye sekta ya elimu.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Stanbic bank Kelvin Winfild ,alisema , Taasisi hiyo ya kifedha moja ya majukumu yake ni kushirikiana na jamii kutoa sehemu ya pato lake ambapo Hadi Sasa imeshatoa kiasi cha sh.Bilioni moja  kusaidia katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu na afya.
Alieleza kwa upande wa watoto katika  Taasisi hiyo ipo nao pamoja , kwa miaka 20 na kuanzia 2018 walianza ujenzi wa madarasa mawili baada ya majengo ya Taasisi hiyo kubolewa Kimara ili kupisha upanuzi wa barabara.
Winfild alisema ,kwasasa wanakabidhi madarasa kumi kati ya Madarasa hayo,  mawili yapo kwenye ukamilishaji.
“Upungufu wa madawati ,sisi Stanbic tulizindua kampeni ya kutoa madawati 1,000 kila mwaka nchini, na Katika kuunga mkono Taasisi hii ya Watoto wetu Tanzania tutawapa madawati 100”.
Kwa upande wake , Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Watoto Wetu Tanzania, Evance Tegete alisema lengo la asasi hiyo Ni kuokoa, kuwalinda na kuwaendeleza watoto wenye Mazingira magumu, waliokuwa wakifanyishwa kazi katika madanguro,kazi za ndani , mashambani,walio lazimishwa kuolewa,na watoto waliotelekezwa.
Tegete alisema, toka kituo kianze  kimesaidia watoto 368 kati Yao 38 wamemaliza degree ,akiwemo binti ambae alikuwa akifanyishwa kazi na Sasa anategemea kumaliza degree yake ya tatu ya sheria .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI