WASIRA AFUNGUA MAFUNZO YA UONGOZI KWA VYAMA SITA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Stephen Wasira, leo Mei 18, 2026, amefungua mafunzo yanayovishirikisha vyama sita vya kihistoria na ukombozi kutoka Kusini mwa Afrika, yakilenga kuimarisha mshikamano, uongozi thabiti, na misingi ya harakati za ukombozi barani Afrika.


Hafla ya ufunguzi imefanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha, taasisi ya pamoja inayomilikiwa na vyama hivyo vya ukombozi kwa ajili ya kujenga uwezo wa viongozi na kuendeleza ushirikiano wa kisiasa na kiitikadi.


Vyama vinavyoshiriki mafunzo hayo ni African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini, Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha Tanzania, FRELIMO cha Msumbiji, MPLA cha Angola, SWAPO cha Namibia, pamoja na ZANU-PF cha Zimbabwe.


Mafunzo hayo yanaendelea kuthibitisha dhamira ya vyama vya ukombozi kuimarisha ushirikiano wao wa kihistoria, kubadilishana uzoefu wa uongozi, na kuandaa kizazi kipya cha viongozi kitakachoendeleza ajenda ya maendeleo, umoja na ustawi wa wananchi wa Afrika. @frelimo_mocambique @officialzanupf @mplaoficial @ccmtanzania









Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

TANZIA;.KWA KHERI DADA YETU MPENDWA EDITHA, TASNIA IMEPATA PIGO

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

NATAKA TANZANIA, KENYE NA UGANDA IWE NCHI MOJA, ILI BAHARI YA HINDI IWE YETU SOTE - MUEVENI

RAIS SAMIA AWASILI IRINGA KWENDA MEI MOSI NJOMBE