Chakula cha Wahadzabe cha matunda na nungunungu Tanzania


Hadza man carrying meat on a stick
Jamii ya Wahadzabe ni moja kati ya makabila yaliyobaki duniani yanayoendeleza shughuli za uwindaji, inadhaniwa kuwa jamii hii imeishi kaskazini mwa Tanzania, ikila matunda na mizizi, na aina mbalimbali za wanyama kwa miaka 40,000.
Mwandishi wa BBC, Dan Saladino alikwenda kuwashuhudia wakikusanya na kuwinda, na kuchunguza iwapo lishe yao ni suluhu kwa matatizo mengi yanayowasibu binadamu kwa sasa.
Angalizo: Baadhi ya picha ni za wanyama waliouawa ni huenda zikawa za kuogofya.
Wakati nikiwa nimelala kifudifudi, niliweka kichwa changu ndani ya shimo lenye giza nikahisi harufu ya mnyama
Lakini sikuamini kuwa mtu ataingia mle ndani na kumtoa mnyama huyo. Mtu huyo ni Zigwadzee, na mnyama alikuwa nungunungu, amini usiamini.
Baada ya kukabidhi uta, mshale na shoka lake kwa mwindaji mwenzake wa Hadzabe, Zigwadzee alishika fimbo fupi iliyochongoka na akaingia shimoni.
Zigwadzee heading down the porcupine hole
Nilifikiri alikua mdogo zaidi kweye kundi lake, na kwa hivyo alikuwa chaguo bora kuingia shimoni. Lakini kadiri nilivyoendelea kuangalia nikagundua kuwa ni kwa sababu Zigwadzee hakua na uoga na chochote pale, hakuogopa aina za nyoka hatari zaidi, kupe na viroboto, na nungunungu wenye miiba yenye urefu wa sentimeta 35.
Hadi hivi sasa chakula changu kutoka jamii ya Wahadzabe kilikuwa ni mboga za majani na matunda tuu. Matunda mengi tuliyachuma katika msitu na vichaka maeneo ya nyika, juu ya miiba na kupitia maeneo yenye nyasi kavu. Wakati mwingine, tungechimbua mizizi kutoka ardhini na kuipika upesi.
Mizizi
Image captionWahadzabe hutegemea sana matunda na mizizi, ambavyo hukusanywa na wanawake
Kulikuwa pia na aina nyingi ya matunda ya mti wa mbuyu. Miti hiyo ya mibuyu huwa na mbegu zinazokuwa ndani ya ganda kama njegere na huwa zimefunikwa kwa kitu chenye weupe unaofanana na vumbi la chaki, na hutumiwa na Wahadzabe kutengeneza kinywaji safi cha nyuzinyuzi chenye vitamini C.
Matunda ya mibuyu yana vitamini C kwa wingi
Image captionMatunda ya mibuyu yana vitamini C kwa wingi
Wataalamu katika historia ya viumbe hai waligundua miongo mingi iliyopita kwamba jamii ya Hdzabe huwa wana njaa mara nyingi lakini kamwe hawawezi kufa njaa. Shauku yao katika suala la kula inasababishwa na kuwepo kwa wingi wa vyakula mbalimbali vinavyowazunguka, lakini changamoto kubwa ipo katika kuweza kupata na mbinu zinazohitajika katika kupata vyakula hivyo.
Maeneo yote yaliyotuzunguka yalikuwa yamesheheni vyakula lakini sisi hatukuweza kuvitambua lakini hata watoto wadogo katika jamii ya hadzabe waliweza kutambua na kupata chakula.
Hadza child eating red meat
Punde nilikuwa tu nasikia sauti ya Zigwadzee kwa mbali, alikua umbali wa futi sita chini ndani ya shimo, ambapo nungunungu alikuwa amejificha, kisha alitoa maelekezo kwa wawindaji wenzake nje ya shimo kuzuia njia zozote ambazo mnyama huyo angeweza kuzitumia kutoroka.
Baada ya dakika 40, alijitokeza tena akiwa amejaa vumbi mwilini na viroboto kadhai, tayari kuchimba chini ya ardhi katika mahali ambapo sasa nungunungu huyo alikuwa.
Hadza
Image captionVijiti hushindiliwa ndani ya magome ya mbuyu ili kuwawezesha kupanda hadi pahali nyuki wamo
Ingawa Wahadzabe ni wachache sana - wanaume, wanawake na watoto 1000 hivi, hivi sasa inaaminika kuwa wale wanaotegemea maisha ya uwindaji pekee ni kati ya 200 na 300, ambao hawalimi wala kufanya aina yeyote ya kilimo.
Jamii hii inawaona wakulima kama wa kushangaza. Mmoja aliniuliza ''kwa nini kusimama shambani siku nzima na kisha kusubiri chakula kwa majuma na miezi wakati unaweza kula matunda ya msituni, kurina asali nyingi ya kula, au kutumia saa moja kufika yalipo maficho ya nungunungu ukalisha familia nzima?"

Hadza man carrying meat and arrows

Hii ndio namna ambavyo mababu zetu walivyokuwa wakijitafutia chakula.
Vyakula ambavyo Zigwadzee na Wahadzabe wenzake hula ndivyo pekee vilivyosalia vyenye uhusiano na vyakula ambavyo mwili wa binadamu ulibadilika na kuvizoea na ndivyo ambavyo vinaufaa mfumo wetu wa kumeng'enya chakula - ikiwa ni pamoja na bakteria ambao sote tunao tumboni na mfumo wa vijidudu vya kinga dhidi ya maradhi viitwavyo kitaalamu Microbiome. Hivi vina uzani wa kilo moja hadi mbili hivi.
Kumekuwa na hali ya kukubaliana katika ulimwengu wa kitabibu kuwa vijidudu hivyo vina kazi kubwa ya kufanya katika mfumo wa kinga, na kuwa kadiri unapokuwa na bakteria hao kwa wingi, hatari ya kupata maradhi hupungua.
Hali kadhalika kwa Wahadzabe, kutokana na aina ya vyakula wanavyovila, wana vijidudu vya aina nyingi sana vya kinga.
Hadza
Image captionMishale yenye sumu huhitajika kuwaua wanyama wakubwa kama vile pundamilia
Pundamilia
Image captionPundamilia huwa rahisi kuua wakati wa kiangazi kwa sababu maeneo ya kunya maji huwa machache
Eating zebra head
Image caption... lakini sasa wameanza kuwa wachache, kwa sababu wanafukuzwa na wafugaji.
Miongoni mwa nilioongozana nao safarini ni Tim Spector, Profesa wa masuala ya kijenetiki katika chuo kikuu cha King's jijini London, ambaye alitaka kubaini iwapo akila kama Wahadzabe, atakuwa na kinga kama yao.
Hivyo alichukua sampuli ya haja kubwa kabla na baada ya siku tatu alipokuwa akila vyakula vya jamii ya Wahadzabe ili kuona kama aina ya vijidudu vinavyosaidia kinga mwilini viliongezeka tumboni mwake.
Matokeo yalikuwa ya kufurahisha. Baada ya siku tatu, aina ya bakteria aliokuwa nao tumboni iliongezeka kwa kiasi cha asilimia 20, na aliweza kugundua aina nadra sana ya bakteria ambao huhusishwa na afya njema mwilini mwake.
Hadza
Image captionWawindaji wakati mwingine hulazimika kusafiri kilomita kadha, wakiwa na windo
Huenda ikachukua miaka kadhaa kwa utafiti wa Spector kufikia majibu halisi kuhusu lishe bora zaidi.
Lakini kuna hali ya dharura kiasi, kwa sababu mambo yanabadilika haraka katika maisha ya jamii ya hadzabe.
Kwa miaka mingi, wakulima wamekuwa wakilima mpaka kuingia maeneo ya ardhi ya Wahadzbe. Katika muongo mmoja uliopita, walikuwa wanafyreka ekari 395 kila mwaka, eneo ambalo Wahadzabe hulitumia kupata chakula.
Wafugaji na ng'ombe wao wenye njaa pia wamekuwa wakiwasili kwa wingi, na kuwafanya wanyama mwitu aina 30 hivi katika maeneo hayo ambao watu wa Wahadzabe wamekuwa wakiwinda na kuwala kwa miaka mingi kutoroka.
hyrax
Kwangu hata hivyo, kuna jambo jingine lililonishangaza zaidi.
Baada ya kuendesha gari kwa dakika 30 hivi kutoka pahala ambapo tulikuwa tumewinda nungunungu, tulipata nyumba iliyojengwa kwa matope na humo ndani mlikuwa na chupa na mikebe iliyokuwa na soda na pakiti za biskuti. Ilikuwa imenuchukua saa tisa kwa gari aina ya Land Rover kufika hapo, lakini nikapata bidhaa hizo zilikuwa zimenitangulia.
Hadza na Coke
Image captionSoda tayari zimefika katika maeneo ya Wahadzabe
Zigwadzee hata hivyo anaendelea kuweka hai ujuzi wa Wahadzabe, ambao ni hakikisho la kifo cha haraka kwa nungunungu.
Ana kwa ana na mnyama, Zigwadzee alimgusa gusa na fimbo huku akimuita ''njoo nungunungu...njoo kwangu...njoo hapa nungu nungu! Kisha, si nungunungu mmoja, mbali walitokea wawili.
Kilichoshangaza zaidi si miiba ya wanjama hao - ambao walikuwa wakubwa sana, wa uzani wa kilo 30 kila mmoja - mbali ilikuwa kelele. Miiba iliinuliwa kwa pamoja na kutoa sauti kali. Zigwadzee aliwagonga nungunungu hao vichwani na muda mfupi baadaye, walikuwa wamekufa.
Zig-wad-zee hitting a porcupine
Wawindaji wa Wahadzabe hugawana kila kitu.
Ni jamii yenye usawa.
Hakuna mifumo ya uongozi na kuhusu nyama, hasa, inapopatikana ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha amegawana na wenzake kwa usalama.
Matumbo, moyo, maini na mapafu yalipikwa papo hapo na kuliwa, lakini nyama hiyo nyingine ilisafirishwa hadi kambini na wakagawana.
Nilipowatazama, huku nikiendelea kula kipande changu cha ini la nungunungu, nilitazama jambo la kipekee. Windo, na chakula, ambavyo viliniwezesha kuwa na uhusiano na utamaduni wa kale sana.
Uta
Image captionNyuta ndivyo vitu pekee mwanamume Mhadzabe humiliki
Picha zote kwa hisani ya Jeff Leach, chuo kikuu cha King's College London

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:

NI HESHIMA KUBWA SANA KUIFUNDISHA YANGA - KOCHA MPYA WA YANGA

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

”RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI”

KOCHA SEAD RAMOVIC AMRITHI GAMONDI YANGA.

UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE