DKT AKWILAPO: IWE MVUA, UPEPO MKALI LAZIMA UJENZI JENGO LA WIZARA YA ELIMU UKAMILIKE KWA WAKATI+video


 Jengo la Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia likavyoonekana baada ya ujenzi wake kukamilika baada ya miaka miwili katika Mji wa Kiserikali wa Magufuli, eneo la Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sazansi na Teknolojia, Dkt Leonard Akwilapo akitiliana saini mkataba na Mkurugenzi wa Mikataba wa Kampuni ya Ujenzi ya CRJE ya China, David Zhou kwa makubaliano ya kampuni hiyo kuanza ujenzi wa jengo la ofisi za wizara awamu ya pili katika Mji wa Kiserikali wa Magufuli eneo la Mtumba, jijini Dodoma. Mkataba huo umesainiwa leo Novemba 24, 2021 jijini Dodoma ambapo ujenzi wa jengo hilo utakamilika kwa miaka miwili na gharama ya ujenzi ni Sh. Bilioni 15.9. Wameteuliwa wasimamizi wa ujenzi huo ambao ni; Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) watakaopatiwa sh. mil. 687.2 na ABEC sh. mir.581.2.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara hizo, Dkt Akwilapo amewaasa wakandarasi kukamilisha ujenzi huo kwa muda uliopangwa bila kusingizia uwepo wa mvua au upepo mkali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt Leonarad Akwilapo akibadilishana hati hizo na Mkurugenzi wa Mikataba wa Kampuni ya Ujenzi ya CRJE ya China, David Zhou.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt Leonard Akwilapo akimkabidhi kitabu cha mwongozo wa ujenzi huo, Mkurugenzi wa Mikataba wa Kampuni ya Ujenzi ya CRJE ya China, David Zhou. Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Moshi Kabengwe.


Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Ujenzi ya CRJE.
Katibu Mkuu, Akwilapo akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo.
Baadhi ya watumishi wa wizara hiyo.



 Katibu Mkuu, Akwilapo (katikati) akiwa na baadhi ya maafisa wa Kampuni ya Ujenzi wa CRJE pamoja na  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Moshi Kabengwe (kushoto),Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo  na Naibu Katibu Mkuu mwingine wa wizara hiyo, Profesa James Mdoe.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ujue yaliyojiri wakati wa kutiliana saini mkataba huo...

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*