TADAYO: SERIKALI IWAJENGEE UWEZO WANASHERIA WA TZ WA KUENDESHA KESI MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI+video
Mbunge wa Mwanga, Joseph Tadayo ameishauri serikali kuratibu mafunzo ya kuwajengea uwezo wanasheria na mawakili wa Tanzania ili wawe na uwezo wa kwenda kuendesha kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki. Aidha, ameishauri serikali kuwajengea pia uwezo wafanyabiashara wa kitanzania ili washiriki kutafuta fursa za aina mbalimbali katika nchi zingine za Afrika Mashariki. Ametoa ushauri wake huo bungeni Dodoma Septemba 20, alipokuwa akichangia hoja kuhusu kuridhia azimio la Bunge kuridhia itifaki ya kuongeza mamlaka ya ya Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Tadayo akitoa ushauri wake huo....
Comments