NMB YATOA VIFAA VYA MICHEZO VYA SH MIL. 24.5 SHIMIWI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko akisalimiana na Meneja Mahusiano Mwandamizi Kati ya Benki na Serikali, Josephine Kulwa (kulia) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Adam Malima (kushoto) na Meneja Mwandamizi Huduma za Kibenki kwa Serikali Benki ya NMB, Amanda Feruzi wakati wa uzinduzi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) katika uwanja wa jamhuri Morogoro huku benki ya ikikabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh24.5milioni.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko akifurahia jambo na naibu waziri wa michezo, utamaduni na sanaa, Hamis Mwinjuma na Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Adam Malima wakati wa uzinduzi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) katika uwanja wa jamhuri Morogoro huku benki ya ikikabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. 24.5milioni.

                                         .................
Michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) imefunguliwa rasmi kuzikutanisha timu zinazowajumuisha  watumishi wa serikali kutoka kwenye wizara, taasisi, wakala za serikali, ofisi za wakuu wa mikoa, halmashauri, pamoja na manispaa.

Uzinduzi huu umefanywa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko aliyeambatana na Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma pamoja Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Adam Malima.

Uwakilishi wa benki umeongozwa na Meneja wetu Mwandamizi wa Mahusiano ya Benki na Serikali, Josephine Kulwa, Meneja Mwandamizi Huduma za Kibenki kwa Serikali, Amanda Feruzi, pamoja na wafanyakazi wengine.








 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

JENGENI UWANJA WA MICHEZO WA KISASA NJOMBE-MWANYIKA

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA