Klabu ya Simba, imethibitisha kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Ndugu Francois Regis, ambaye alikuwa ni Mtendaji Mkuu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa klabu hiyo huku ikimshukuru Mr. Regis kwa kipindi alichohudumu klabuni hapo.
Taarifa ya leo Novemba 23, 2024 iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza kwamba bodi ya Simba Sc imefanya uteuzi wa Bi. Zubeda Hassan Sakuru kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu.
“Bi. Zubeda yuko mbioni kuhitimu Shahada yake ya kwanza ya Uzamivu, ana Shahada mbili za Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza na Chuo Kikuu cha Mzumbe Tanzania. Pia ana Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.” ——imesema taarifa hiyo
“Bi. Zubeda amefanya kazi kama Meneja Miradi wa Simba akimsaidia Bw. Kajula kuhusu mchakato wa kutengeneza sera na ushauri wa masuala ya kiutendaji.”——imesema
Comments