CPL. MWIKWABE AKABIDHI KITI MWENDO KWA MTOTO MWENYE ULEMAVU WA KUZALIWA

 Polisi Kata ya Ikoma Tarafa ya Grumet wilayani Serengeti mkoani Mara, CPL. Emmanuel Mwikwabe amekabidhi kiti mwendo kwa mtoto Vaileth Enock(16) mwenye ulemavu wa kuzaliwa ambao umepelekea kupooza.

CPL. Mwikwabe alimbaini Mtoto huyo kupitia kampeni ya utoaji wa Elimu ya Polisi Jamii Nyumba kwa Nyumba katika Kijiji cha Parknyigoti kitongoji cha Park B kupitia Baba yake mzazi Mzee Enonck Komanya.

“Nilifanikiwa kufika nyumbani kwa Mzee Enonck Komanya nakuwakuta watoto miongoni mwa watoto niliowakuta kwenye mji huo ni pamoja na Binti huyu Vaileth na ndipo nikaamua nimshirikishe Mkuu wa Wilaya Bi.Kemirembe na kukubali kunishika mkono kwa kunipa kiti mwendo,”alisema CPL. Mwikwabe.

Pia amesema nimekabidhi kiti hicho nakupeleka faraja kwa Mtoto huyo ambaye tangu azaliwe amekuwa akiishi kwa kulala kutokana na kukosa kiti mwendo.

Mwikwabe amewataka Wazazi pamoja na wakazi katika kata hiyo kuacha kuwabagua watoto wenye ulemavu waliopo kwenye maeneo yao kwani kufanya hivyo nikuwafanyia ukatili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:

NI HESHIMA KUBWA SANA KUIFUNDISHA YANGA - KOCHA MPYA WA YANGA

UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI

”RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI”

KOCHA SEAD RAMOVIC AMRITHI GAMONDI YANGA.

TAMISEMI PUUZENI DOSARI NDOGONDOGO ZA WAGOMBEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA - DK. NCHIMBI

RAIS SAMIA ATOA SALAMU ZA POLE KWA KIFO CHA DKT. NDUGULILE

CCM YASAMBAZA VIONGOZI NA MAKADA WAANDAMIZI NCHI NZIMA