“Hii ni sababu inayotofautisha Chama Cha Mapinduzi na vyama vingine, hivyo endeleeni kukiamini Chama Cha Mapinduzi kama mlivyokiamini mwaka 2019 na sasa tumerudi kuwaeleza yale tuliyoyafanya na kwanini tunaomba tena ridhaa ya kuongoza katika ngazi ya Mitaa, Vijiji na Vitongoji 2024” Amesema Komred Nape.
Aidha, komredi Nape amewasisitiza viongozi waliochaguliwa kwenda kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi, wafanye kampeni za kisayansi na kistaarabu bila kuwatukana vyama vingine.
“Wakiwashambulia kwa matusi waacheni kwa sababu wameshaanza wenyewe kupasuana ndani kwa ndani na muda siyo mrefu watagawana Mbawa” Amesema Komredi Nape.
“Ndugu wananchi na wanachama pamoja na viongozi tunaomba mkakichague Chama Cha Mapinduzi kwa sababu hakuna Chama kingine kinachoweza kuwaongoza na kuwaletea maendeleo wananchi isipokuwa Chama Cha Mapinduzi pekee, huko kwingine wanagombana hivi karibuni watagawana Mbawa” Amesema Komredi Nape.
Komredi Nape ameielekeza Serikali kuweka utaratibu mzuri wa kuwalipa wananchi fedha zao zaidi ya Sh.Bil. 21 ndani ya mwezi huu wanazodai kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA ) unaojishughulisha na ununuzi wa mazao hapa Rukwa.
“Nimeongea na Waziri wa Kilimo, Ndugu Hussein Bashe amenihakikishia ndani ya mwezi Novemba atawalipa wakulima na wafanyabiashara wa mahindi ambao wanadai madai yao tangu walipouza mazao yao na kutokulipwa hadi sasa, na zoezi la ununuzi litaendelea hadi Mwezi Februari 2025” Amesema Komredi Nape.
Pamoja na mambo mengine Komredi Nape akiwa katika Mkoa wa Rukwa wilaya ya Sumbawanga Mjini amezindua Shina la kikundi cha Umoja wa Madalali wa Maroli Sumbawanga.
Kikundi hicho kimetoa mwelekeo wa namna watakavyoendesha shughuli zao za kujipatia kipato na kusaidiana katika Shida na Raha kwa kuomba tenda zote zinazohusu usafirishaji zinazopatikana katika manispaa ya Sumbawanga.
Nae komred Nape alipokea na kutoa maelekezo kwa Kamisaa wa wilaya na kuwaeleza vijana hao wasajili kampuni ili waweze kuwa Rasmi kupata tenda za hapa Mjini kama walivyoomba.
Mgeni Rasmi ambae ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa amekutana na kamati ya siasa Mkoa wa Rukwa pamoja na kufanya kikao cha ndani na Kamati zote za siasa za wilaya na Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Sumbawanga Mjini na kumaliza kwa kufungua Rasmi Mikutano ya Hadhara itakayoendelea katika Mitaa, vijiji na vitongoji Katika Ufunguzi wa Mkutano wa Kampeni za Serikali za Mitaa 2024 uliofanyika 20 Nov 2024 Mkoani wa Rukwa.
Komredi Nape akiwa na viongozi wengine wa chama wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo.
Comments