Wenyeviti na wajumbe wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji wa Kata Ramadhani wakila kiapo cha uadilifu na uaminifu mbele ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Njombe, Isack Mlowe baada kuwa washindi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda mitaa yote 9 ya Kata hiyo iliyopo Njombe Mjini.
Katibu Mwenezi Mstaafu wa CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole ambaye alikuwa miongoni mwa wana CCM walioendesha harakati za kuhakikisha wagombea wa CCM wanashinda akiwa na Diwani wa Kata hiyo, Dkickson Nganyange wakati wa uapisho huo.
Viongozi hao wakijaza na kutia saini kwenye fomu za kiapo.
Dickson Nganyange Diwani wa Kata ya Ramadhani akitoa nasaha kwa viongozi hao.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MSIMAMIZI MKUU KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV 0754264203
Comments