Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile (katikati) akimjibu mwananchi aliyepiga simu kutaka kufahamu utaratibu wa kuwasilisha malalamiko EWURA.
Namba ya huduma kwa wateja itakayokuwa inatumika kupiga simu BURE ni 0800110030 ambapo tofauti na awali, mpokeaji wa simu alitakiwa kuwa na simu ya mezani, kwa sasa mawasiliano hayo yatapokelewa moja kwa moja kwenye kompyuta.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile amezindua mfumo huo kwa kuhudumia wateja moja kwa moja waliopiga simu kufahamu masuala mbalimbali ya kiudhibiti kwenye sekta zinazodhibitiwa na EWURA za nishati na maji.
“Leo tunapozindua mfumo huu wa kidigiti, iwe chachu kwetu kutoa huduma kwa wateja kwa ufasaha na ufanisi zaidi na popote ambapo mtoa huduma atakuwepo ulipo mtandao”. Alisisitiza.
Kwa kuzinduliwa mfumo huu, mteja yeyote anaweza kupiga simu EWURA kwa namba 0800110030 bila makato, kwa siku za kazi, Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri.
Comments