ZAIDI YA MIRADI 2000 IMESAJILIWA AWAMU YA RAIS SAMIA

Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan  TIC imesajili miradi 2,020, ambayo ni ongezeko la asilimia 91 ikilinganishwa na miradi 1,057 iliyosajiliwa katika kipindi cha 2017-2020. 

Thamani ya mitaji ya miradi hii inakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 23.67, ikiongezeka kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2 katika kipindi cha 2017-2020. Aidha, miradi hii inatarajiwa kutoa Ajira zilizozalishwa kutokana na usajili wa miradi kumekuwa na ongezeko la Asilimia 284.5 kutoka ajira 136,232 zilizozalishwa kipindi cha miaka minne ya kuanzia mwaka 2017 mpaka 2020 mpaka ajira 523,891 zinazotarajiwa kuzalishwa katika kipindi cha miaka minne ya awamu ya sita kuanzia 2021-2024.


Mafanikio hayo yametajwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika mkutano wa kuelezea mafanikio ya taasisi hiyo  iliyoyapata kwa mika minne katika Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia kweny Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Februari 27, 2025.


"Kumekuwa na ongezeko la usajili wa miradi kutoka nje linalotokana na juhudi zinazofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuitangaza nchi na kuhamasisha uwekezaji kupitia sera yetu maalum ya mashirikano kupitia Diplomasia ya kiuchumi. Na pia ongezeko la miradi linatokana na ushiriki wa Tanzania katika makongamano mbalimbali nje ya Nchi na maboresho mbalimbali yanayofanywa na Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini." Amefafanua Teri.


Amesema kuwa thamani ya mitaji ya miradi iliyosajiliwa imepanda kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2 hadi bilioni 23.67, ishara ya kuongezeka kwa uaminifu wa wawekezaji kwa serikali ya Awamu ya Sita.

3.1 Usajili wa Miradi ya Uwekezaji

Aidha, Teri amefafanua kuwa katika kipindi mwaka Januari 2021 hadi Januari 2025 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kusajili jumla ya miradi 2,020 ambayo ilikadiriwa kuwekeza kiasi cha mtaji wa Dola za Marekani bilioni 23.67 na kutoa jumla ya ajira 523,891. Kati ya miradi hiyo asilimia 35 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya Wageni na asilimia 23.1 ni ya ubia kati ya Watanzania na Wageni. 


Teri aliendelea kueleza kuwa, tathmini inaonesha kuwa idadi kubwa ya miradi iliyosajiliwa ipo katika sekta za kipaumbele ambazo ni: Uzalishaji viwandani miradi  538 (45.29%), Usafirishaji miradi 225 (18.94%), Utalii miradi 110 (9.26%),  sekta ya ujenzi wa majengo ya biashara miradi 106 (8.92%) Kilimo miradi 106 (8.50%), kama inavyoonesha katika Jedwali Na. 1.Jedwali Na.1: Mwenendo wa Uwekezaji kwa kipindi cha Januari 2021 - Januari 2025 


Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bw. Gilead Teri akitoa taarifa ya utekelezaji na mafanikio ya kituo hicho ndani ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa Waandishi wa Habari ikiwa ni programu iliyoandaliwa na Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Februari 27, 2025.


Mkurugenzi Msaidisi wa Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa akitoa neno la utangulizi alipokuwa akimkaribisha Teri kuzungumza na vyombo vya habari.

Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini wakati wa mkutano huo.

Zamaradi Kawawa akizungumza na waandishi wa habari na kuwapa utaratibu na ratiba za mikutano hiyo ya Taasisi.

Zamaradi Kawawa akimsindikiza Teri baada ya mkutano kumalizika.


 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

MSIMAMIZI MKUU

KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV

0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO 8 MWANAMKE HUFANYA KWA MWANAUME ANAYEMPENDA