Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mabadiliko ya tarehe ya Kamati Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutangaza majina matatu kati ya waliotia nia kuwania ubunge kupitia Chama hicho.
...........
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza Julai 28 mwaka huu kuwa siku ya mwisho ya kutoa majina ya uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Ubunge, Udiwani na uwakilishi baada ya kukamilisha mchakato huo na kuwataka wagombea kuwa watulivu.
Pia kimesema kutakuwa na kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitakachofanyika Julai 26 mwaka huu kikitanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya Chama hicho.
Taarifa hiyo imetolewa jijini Dodoma leo Julai 19/2025 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mabadiliko ya tarehe ambapo majina yalikuwa yatangazwe Julai 19/ 2025.
Kwa muktadha huo, CCM imewataka wagombea kuwa watulivu wakati ikiendelea kukamilisha mchakato huo kwa kuwa idadi ya wagombea ni kubwa na wao wanataka kufanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa.
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments