Baba ndiye anayepaswa kuwa na taswira ya wapi familia inaelekea — katika masuala ya:
- Kiuchumi (maendeleo ya mali, makazi, elimu ya watoto)
- Kiimani (mafundisho ya kiroho, maombi, kumcha Mungu)
- Kijamii (mshikamano, heshima na mafanikio ya kifamilia)
Uthibitisho wa Kimaandiko:
- Waefeso 5:23 — “Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe...”
- Mithali 29:18 — “Pasipo maono, watu hujiachilia...”
- Mwanzo 18:19 — “Maana nimemjua Ibrahim, kwamba atawaamuru watoto wake na nyumba yake baada yake, wayashike njia za Bwana...”
Mwanaume wa kweli si yule anayetoa amri kwa sauti, bali yule anayetoa mwelekeo kwa maono.
Baba wa kweli huamka mapema kuombea familia yake, huona mbali hata watoto wake wasipoona, hujinyima ili familia iendelee.
Comments