TANZANIA KUWA KITOVU CHA USALAMA WA CHAKULA AFRIKA 2050


 Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025–2050 imeweka mkakati madhubuti wa kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usalama wa chakula barani Afrika. Kupitia mageuzi katika sekta ya kilimo, nchi imeweza kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha utoshelevu kwa kiwango kikubwa.


Katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili, bajeti ya sekta ya kilimo imeongezeka kwa kasi kubwa — kutoka TZS bilioni 50 mwaka 2000/2001 hadi kufikia TZS trilioni 1.24 mwaka 2025. Ongezeko hili limechochea uwekezaji katika pembejeo, miundombinu ya umwagiliaji, tafiti za kilimo, pamoja na upatikanaji wa masoko ya uhakika.


Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2014/2015 uzalishaji wa mazao ya chakula ulikuwa tani milioni 16, na kiwango cha utoshelevu kilikuwa asilimia 125. Mwaka 2020/2021 uzalishaji ulifikia tani milioni 17.5, na hadi mwaka 2024/2025 umeongezeka hadi tani milioni 22.8 — sawa na ongezeko la asilimia 33 ndani ya miaka minne.


Hali hii imeiwezesha Tanzania kuwa na utoshelevu wa chakula wa asilimia 128, hatua inayoweka msingi imara wa kufikia utoshelevu endelevu na hatimaye kuifanya nchi kuwa kitovu cha uzalishaji na usambazaji wa chakula kwa nchi nyingine barani Afrika ifikapo mwaka 2050.


Kwa mujibu wa Dira ya Taifa, mwelekeo huu utaiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache Afrika zitakazokuwa na uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha, si tu kwa matumizi ya ndani bali pia kwa kuuza nje hivyo kuchangia usalama wa chakula kimataifa.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

CHINYELE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE DODOMA MJINI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.