UPATIKANAJI WA MAJI SAFI KIGOMA UMEKIA ASLIMIA 77 - RC SIRRO

 Huduma za upatikanaji wa maji safi zimefikia asilimia 77 mwaka 2025 ambapo vijiji 246 vimefikiwa kupitia mtandao wa bomba na vijiji 44 vinapata maji kupitia visima na chemichemi zilizoboreshwa


Miradi 91 imekamilika na kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi wapatao 1,456,116 na kuendelea na utekelezaji wa miradi 20 iliyo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, IGP mstaafu, Balozi Simon Sirro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Julai 19, 2025, kuhusu mafanikio ya mkoa huo katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


"Serikali imeongeza kasi ya uchimbaji wa visima vya maji kutoka visima 49 mwaka 2020 hadi visima 101 mwaka 2025," amesema Sirro na kumpongeza Rais Samia kwa kuujali kimaendeleo mkoa wa Kigoma.

RC Sirro akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Rodney Thadeus akitoa neno la utangulizi alipokuwa akimkaribisha mkuu huyo wa mkoa.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

MSIMAMIZI MKUU

KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV

0754264203


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

DIARRA KIPA BORA TANZANIA

CHINYELE ACHUKUA FOMU KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE DODOMA MJINI

MAKUNDI YA VILABU VINAVYOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2025.