*WANAWAKE MNANISKIA AMA NIONGEZE SAUTI*
🍃🪨▫️ kati ya mwanamke na mwanaume, tunakubaliana kwa pamoja kwamba, wanaume ni viumbe rahisi mno kuridhishwa kwenye suala la tendo la ndoa.
🍃🪨▫️Mwanzoni, kitu kinachomhamasisha mwanaume ni muonekano wako tu wa kimahaba (kwa mwanamke).
🍃🪨▫️Lakini kadiri siku zinavyosonga mbele kwenye ndoa, inakuwa ngumu kupandisha munkari wake, hata kama wewe ni mwanamke mrembo kiasi gani.
🍃🪨▫️Kumridhisha mwanaume wako inaweza ikawa rahisi kama tu utakumbuka kuweka mambo katika hali ya mvuto (remember to keep things interesting).
🍃🪨▫️Tafuta namna ya kuleta hamasa kama ile iliyokuwepo siku za mwanzomwanzo wa penzi lenu.
🍃🪨▫️ Kwa uhakika utakamata usukani. Pamoja na kumheshimu, kama mtazingatia sheria zifuatazo kwa makini, basi mwanamke hatakuwa na shida ya kumridhisha mumeo.
*VAA VIZURI*
🍃🪨▫️Utamu wa faragha unaweza ukawa kwenye tendo lenyewe, lakini matamanio ya kufanya tendo hilo, yanategemeana na mambo mengine mengi.
🍃🪨▫️ Vaa vizuri wakati wa kulala, wakati wote na siyo tu wakati wa usiku, ambao unataka kufanya tendo.
🍃🪨▫️Vaa nguo nyororo, yenye mtelezo unaomwagika mwilini.
🍃🪨▫️Kwa vazi hili na mtembeo wa kimahaba chumbani, mwanaume wako hatataka kutoa mikono yake mwilini mwako.
🍃🪨▫️Siyo unavaa vizuri tu ukiwa unakwenda sokoni na kwenye ibada, lakini nyumbani unajisahau
*AIBU TUPA KULE*
🍃🪨▫️Usiwe mtu wa aibuaibu linapokuja suala la tendo.
🍃🪨▫️Mwanaume anaweza akakupenda kwa mapozi yako na aibu kwanza (lugha iliyotumika hapa ni ‘innocence’), lakini hakuna mwanaume atakayeendelea kuvumilia mwanamke ambaye anashtushwa kirahisi na kila kitu (mitindo ya tendo).
🍃🪨▫️Wanaume wanapenda wanawake, ambao ni wataalam kwenye faragha.
🍃🪨▫️ Wanaume wanapenda wanawake, ambao wana manjonjo mbalimbali wakati wa shughuli.
🍃🪨▫️Kama unataka kumridhisha mwanaume wako, basi jitahidi ujue mbinu ambazo zinatumiwa kitandani.
🍃🪨▫️ Siyo akikuambia fanya hivi, unaanza eti hizo staili za wanawake wako usiniletee, akikuambia fanya hivi, eti sitaki, kwanza niache nmechoka! Mwanaume hatakujibu kwa maneno, bali vitendo.
*FANYA MAZOEZI*
🍃🪨▫️Wanaume ni watu wa kujali sana mwonekano wa mwanamke.
🍃🪨▫️Kwa hiyo siyo lazima kuonekana kama walimbwende, lakini mtazamo wa karibu na hapo, utakuongezea mvuto zaidi.
🍃🪨▫️Ndiyo, mwanaume wako anakupenda kama ulivyo, lakini lazima tuukabili ukweli kwamba watu wenye kufanya mazoezi wanaonekana na mvuto zaidi, hakuna kupinga hilo.
🍃🪨▫️Hakikisha shughuli yako siyo ya kitoto unapokuwa kwenye kumi na nane.
🍃🪨▫️ Siyo dakika mbili tu unahema kiasi kwamba unashindwa hadi kuendesha farasi.
*KUWA MCHOKOZI*
🍃🪨▫️Hapa haimaanishi ule uchokozi wa kuleta ugomvi la hasha! Bali ni ule uchokozi, ambao kwa lugha ya Kiingereza unafahamika kama ‘tease’ kwa maana hiyo, basi tunasema ‘tease him’.
🍃🪨▫️Cheza naye michezo mbalimbali na uburudike naye ipasavyo.
🍃🪨▫️ Kumbuka michezo isiwe ya kitandani tu, kama karata na kadhalika, bali michezo ya hata nje ya kitanda kama kukimbia na kucheza kidali po!
🍃🪨▫️Kama unataka kuwa mjuzi kwenye faragha, basi unatakiwa umfanye mwanaume wako akutake wakati wote na popote.
🍃🪨▫️Tendo la ndoa siyo swichi ambayo unawasha na kuzima mnapokuwa chumbani tu.
🍃🪨▫️ Mchokoze chokoze katika mitindo ya kimahaba bila kuvuka mipaka.
🍃🪨▫️Hata kama mmekwenda kwenye matembezi na kuchanganyikana na familia au marafiki zenu, mkonyeze, mtege, usiogope kumpapasa kisiri, ringaringa na kujidekeza.
*JIAMINI NA JIPENDE*
🍃🪨▫️Ndiyo, utaonekana vizuri zaidi ukipunguza unene, lakini hiyo haimaanishi kwamba haupo bomba.
🍃🪨▫️ Hakuna kinachokera wanaume, kama mwanamke ambaye anauonea aibu mwili wake mwenyewe anapokuwa faragha.
🍃🪨▫️ Jiamini kuhusu mwili wako na jaribu mambo mbalimbali na mwanaume wako.
*NIMEMALIZA*
#hdmasterplan
Comments