Taarifa kwa umma kuhusu kukamilika kwa zoezi la uteuzi wa
wagombea wa nafasi ya Spika
1.0 zoezi la Uteuzi wa Wagombea wa Uchaguzi wa Spika limekamilika
tarehe 10 Novemba, 2025 saa 10:00 Alasiri. Napenda kuchukua
nafasi hii kuwafahamisha yale yaliyotokana na zoezi hili na
mchakato mzima toka tulipoanza, tulipo na tunapoelekea.
2.0 Uchaguzi wa Spika unafanywa kwa mujibu wa lbara ya 86 (1) ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977,
Kanuni ya 9 na Nyongeza ya Kwanza ya Kanuni za Kudumu za
Bunge, 2025.
3.0 ili kukidhi matakwa hayo, tarehe 4 Novemba, 2025 nilitoa Tangazo
namba 14824A katika Gazeti la Serikali Toleo Maalum Namba 11
kuvijulisha vyama vya siasa vyenye usajili w a kudumu
vinavyokusudia kusimamisha mgombea katika uchaguzi huo
Kufanya Mchakato na kuwasilisha jina la mgombea husika ofisini
kwa Katibu wa Bunge Dodoma kabla ya saa 10.00 jioni ya tarehe
10 Novemba, 2025 ambayo ndio siku ya uteuzi
4.0 Hadi kufikia saa 10:00 Alasiri leo tarehe 10 Novemba, 2025
Wagombea waliowasilishwa na Vyama vyao ni kama ifuatavyo:-
Mhe. Mussa Azzan Zungu kutoka Chama cha Mapinduzi
(CCM);
Ndg . Veronica Charles Tyeah kutoka Chama cha National
Reconstruction Alliance (NRA);
Ndg. Anitha Alfan Mgaya kutoka Chama cha National
League for Democracy (NLD):
Ndg Chrisant Nyakitita kutoka Chama cha Democratic Party
(DP)
Ndg. Ndonge Said Ndonge kutoka Chama cha Alliance for
Africa Farms Party (AAFP): na
Ndg. Amin Alfred Yango kutoka Chama cha Aliance for
Democratic Change (ADC).
5.0 Baada ya uchambuzi uliozingatia nafasi ya Kiti cha Spika, sifa za
wagombea waliopendekezwa na vyama na matakwa mengine ya
Kisheria na Kikanuni nimeridhika kwamba Wagombea wote
wametimiza masharti ya Kanuni
Uchaguzi. Hivyo,
za
nimewaidhinisha wagombea hao sita waliowasilishwa kwangu.
6. 0 Hivyo, bila kuathiri Shughuli nyingine zitakazopangwa na Bunge
tarehe 11 Novemba, 2025 saa Tatu asubuhi au muda mfupi baada
ya hapo, nitawasilisha majina ya Wagombea walioteuliwa kwa
Wapiga kura ambao ni Wabunge Wateule wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ili Uchaguzi ufanyike kwa mujibu wa
utaratibu utakaotolewa wakati wa Uchaguzi
7.0 Napenda kutoa shukrani kwa Vyama vya Siasa vinavyohusika na
Wagombea wote kwa ushirikiano mlionipa katika kukamilisha zoezi
la Uteuzi.
Baraka I. Leonard
KATIBU WA BUNGE NA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI
10 Novemba, 2025

Comments