UCHAGUZI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa tarehe 29 Oktoba 2025 ulikuwa sehemu ya historia ya maendeleo ya demokrasia ya vyama vingi tangu mwaka 1992. Mamilioni ya Watanzania zaidi ya milioni 31.7 walijitokeza kwa amani kutekeleza haki yao ya kikatiba, ingawa baadhi ya maeneo kama Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Songwe yalishuhudia matukio ya uvunjifu wa amani, uporaji, kuchoma moto mali za umma na binafsi kwa kisingizio cha kudai haki.
Kuanzia siku ya uchaguzi na siku chache baadae, vurugu zililipuka: vituo vya mafuta vilichomwa moto, magari ya mwendokasi na vituo vyake vikaharibiwa, ofisi za serikali na vituo vya polisi vikaathirika, mali binafsi zikaporwa na kuharibiwa. Jeshi la Polisi na vikosi vya usalama vililazimika kudhibiti hali, maeneo kadhaa yakatiwa ulinzi maalum na mawasiliano ya kidigitali yakadhibitiwa kwa muda mfupi kuzuia taarifa za uchochezi.
Uchochezi kutoka mitandao ya kijamii
Uchunguzi umebaini kuwa machafuko hayo hayakuwa ya bahati mbaya. Mitandao kama X (Twitter), TikTok, Facebook, na WhatsApp ilitumika kuratibu vurugu kupitia video na sauti za uchochezi. Akaunti nyingi zilitoka nje ya Tanzania, hasa Kenya, ambako watumiaji walionekana kushabikia vurugu na kupotosha umma kuhusu matokeo ya uchaguzi.
Sababu za Kenya kuchochea machafuko Tanzania
Swali linaibuka kwa nini Kenya? Wala si kwa sababu ya ujirani au mapenzi kwa demokrasia. Ukweli unajificha katika ujasusi wa kiuchumi (economic espionage) na ushindani wa kimkakati wa bandari kati ya Tanzania na Kenya.
Kwa miaka mingi, Bandari ya Mombasa imekuwa lango kuu la biashara Afrika Mashariki, lakini mageuzi ya Bandari ya Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Dubai Ports World (DP World) yamebadilisha hali. Kupungua kwa muda wa kushusha mizigo kutoka siku 5 hadi 1, kuondolewa kwa ada nyingi, na utekelezaji wa Dar es Salaam Maritime Gateway Project (DMGP) yenye thamani ya dola milioni 420, vimeifanya Tanzania kuvutia wafanyabiashara wengi.
Mradi wa reli ya kisasa (SGR) unaounganisha Dar es Salaam na Isaka–Kigoma unaongeza ufanisi katika usafirishaji wa mizigo kwenda DRC, Burundi, Zambia, Malawi na Rwanda. Hali hii imesababisha wafanyabiashara wengi kuhamisha mizigo yao kutoka Mombasa kwenda Dar es Salaam.
Ushindani wa bandari na hasara kwa Kenya
Ripoti ya East African Business Review (2024) inaonyesha kuwa Uganda, Rwanda, Burundi na DRC wameanza kutumia Bandari ya Dar es Salaam kutokana na gharama nafuu. Bandari ya Mombasa imeanza kupoteza mizigo — takwimu za 2023 zinaonyesha kushuka kwa 1.9% katika shehena iliyoshughulikiwa. Hii imeilazimisha Kenya kupunguza ada na kutoa motisha mpya kwa wateja wake.
Hofu ya Kenya: Tanzania inainuka
Tanzania sasa inakua kwa kasi kubwa kiuchumi. Kiwango cha ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) ni 6.1% ikilinganishwa na 4.5% cha Kenya (Benki ya Dunia, 2024-2025). Sekta za madini, nishati, bandari na ujenzi zimeifanya Tanzania kuwa kitovu kipya cha uwekezaji Afrika. Kenya, kwa kuona tishio hili, inafaidika ikiwa amani ya Tanzania itavurugika jambo linaloweza kupunguza imani ya wawekezaji.
Vita baridi ya kiuchumi kupitia mitandao ya kijamii
Mitandao imekuwa uwanja wa vita mpya. Nchini Kenya, watengeneza maudhui na “influencers” wanaweza kufadhiliwa kueneza taarifa za kupotosha. Oxford Internet Institute (2023) iliripoti Kenya kama moja ya nchi 10 za Afrika zenye kampeni za mitandao zilizopangwa kisiasa (orchestrated social media campaigns).
Siku ya uchaguzi wa Tanzania, kurasa nyingi za mitandao kutoka Kenya zilieneza picha na video za uongo zikionyesha kana kwamba Tanzania “imeingia machafuko”. Vyombo vya habari vya Kenya navyo vilishiriki kusambaza propaganda hizo kwa kutumia picha za zamani na video kutoka nchi nyingine, zikilenga kupaka tope sifa ya Tanzania kimataifa.
Majibu ya vyombo vya usalama vya Tanzania
Licha ya presha hiyo, vyombo vya usalama vya Tanzania vilidhibiti hali kwa ustadi mkubwa. Dar es Salaam ilirejea kuwa tulivu ndani ya saa 48. Jeshi la Polisi, JWTZ, TISS na FFU walifanya kazi kwa ufanisi bila kutumia nguvu kupita kiasi, huku wakilinda haki za raia. Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ilionesha uthabiti na ukomavu, ikionyesha dunia kuwa Tanzania si taifa dhaifu linaloweza kuchezewa na mitandao.
Hitimisho
Machafuko ya Oktoba 29, 2025 hayawezi kuelezwa kama tukio la kisiasa pekee, bali ni sehemu ya vita baridi ya kiuchumi katika Afrika Mashariki. Tanzania inainuka kama nguvu mpya ya biashara, huku Kenya ikihofia kupoteza nafasi yake ya kihistoria. Hivyo, kampeni za mitandao, uchochezi wa kidigitali na hoja za “kupigania demokrasia” zinaweza kuwa mbinu za kuzuia kasi ya Tanzania kupaa kiuchumi.
Ndugu zangu Watanzania tunaweza kutofautiana kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiitikadi lakini kama taifa hatupaswi kugawanyika.
Kenya inapakana na mataifa yenye changamoto nyingi za kidemokrasia lakini kwanini wamechagua kuisemea Tanzania? Kwa sababu sisi ni washindani wao kiuchumi.
Kenya inapakana na Uganda, Sudan Kusini na Somalia mbona hawashobokei siasa za mataifa hayo?
Mwaka 2007 zaidi ya Wakenya 3000 waliuawa kwenye uchaguzi na mbona hatukuwashobokea, Ndugu zangu Watanzania tusiichezee amani yetu na tunaweza kuingia kwenye vita ya propaganda na kujikaanga kwa mafuta yetu wenyewe.
Kenya ni kibaraka wa mabeberu ambaye ametumwa kuhujumu uchumi wetu na amani yetu. Kenya kuna kambi tano za majeshi kutoka Marekani na Uingereza.
Kenya ni taifa ambalo limejengwa kwa misingi ya udalali wa Kimataifa.
Kenya wanafanya biashara na waasi wa M23 kutoka Kongo kinyume na makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC na SADC, Kenya wamewahi kufanya mkutano na waasisi wa RSF kutoka Sudan kinyume na makubaliano ya Umoja wa Afrika.
Kenya hana nia njema na Tanzania,yeye ni mshindani wetu kiuchumi hivyo anatumia turufu muhimu ya mipasuko yetu kujinufaisha .

Comments