Mwishoni mwa mwaka, swali muhimu si mwaka umekuwaje?
Bali ni Nimekuwa nani ndani ya mwaka huu?
Maswali haya saba yatakusaidia kupima safari yako, kuelewa mwelekeo wako, na kupanga upya kwa hekima..
1. NIMEFANIKIWA WAPI?
Tazama maeneo yote ya maisha yako kazi, fedha, imani, mahusiano, afya, tabia, na malengo binafsi. Tambua ushindi hata kama ni mdogo
kila hatua mbele ni ushindi.
2. NIMEKOSEA WAPI?
Tambua makosa bila kujilaumu.
Huwezi kurekebisha kitu usichokikiri.
Makosa ni data ya kukusaidia kufanya maamuzi bora mwaka unaofuata.
3. NIMEJIFUNZA NINI?
Kila tukio zuri au baya linabeba somo.
Je, mwaka huu umejifunza kuhusu tabia yako? watu?pesa? kazi? Mungu?uvumilivu?nk.Maarifa unayobeba kutoka mwaka huu ndiyo mtaji wa mwaka ujao.
4. NANI AMENIINUA?
Tafakari wale waliokutia moyo, waliokuongoza, waliokupa nafasi, waliokuombea, au kukusaidia.
Hao ndio watu wa kuongeza kwenye mduara wako wa ukuaji. Mafanikio hutembea kwa miguu ya watu sahihi.
5. NANI AMENIRUDISHA NYUMA?
Je, kuna watu au mazingira yaliyokuondoa kwenye malengo? Tamaa mbaya?Mazingira yenye kelele? Mahusiano yenye sumu?Watu wasioshikika?
Hili si swali la kuhukumu, bali la kuamua ni nani wa kumweka karibu mwaka ujao.
6. NINI NAHITAJI KUBADILISHA?
Huwezi kupata matokeo mapya kwa kutumia tabia zile zile.
Je, ni Nidhamu ya kifedha?Ratiba yako?Mazingira yako?Mitazamo yako?Muda unaotumia mtandaoni? Tabia unazozilea?
Ukuaji huanza pale unapobadilisha kile kinachokuzuia.
7. NIANZIE WAPI TENA?
Usiingie mwaka mpya bila mpango.
Tengeneza hatua ya kwanza, sio orodha ndefu. Anza na jambo moja muhimu. Anza na tabia moja mpya au biashara kufanikisha
Unachokianzisha Januari kinaamua unachovuna Desemba.
Maswali haya ni dira ya kuhakikisha unaingia mwaka mpya ukiwa thabiti, mwelekeo ukijulikana, na malengo yakiwa wazi kwa mafanikio 2026.
Ni jambo gani bado linakusumbua kati ya haya?. Niandikie hapa chini kwenye comment ili niweze kukusaidia.
#professoranoldfanue0714577147 #DarEsSalaamBusiness #daressalaamtanzania

Comments