SERIKALI YAENDELEA KUKUTANA NA VIONGOZI WA DINI, TEC NA WA KIMILA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema serikali imeendelea kufanya mikutano na viongozi wa taasisi mbalimbali za dini, ikiwemo Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), na viongozi wa kimila ili kuwaeleza hali halisi ya usalama nchini na kuwataka kuendelea kudumisha amani.

Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na wananchi wa Arusha katika ziara yake ya kikazi ambayo pia ameitumia kuangalia uharibifu uliofanywa katika vurugu ya Oktoba 29.

Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa amani kama msingi mkuu wa maendeleo ya taifa.

Katika ziara hiyo pia  aliwapa wananchi salamu za pole zilizotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia athari za  vurugu zilizotokea hivi karibuni.

Waziri Mkuu alitembelea na kukagua uharibifu uliotokea wakati wa vurugu za Oktoba 29, 2025, ambapo Kituo cha Polisi cha Kikatiti, Mahakama ya Mwanzo ya Maji ya Chai, na kituo cha mafuta cha Total Energies vilichomwa moto. Aidha, alibaini kuibwa kwa mali katika soko kuu na kubomolewa kwa sefu ya kutunzia fedha.

Waziri Mkuu amewaonya wananchi kuwa kuchagua vurugu ni sawa na kuchagua kufukuza maendeleo na kuongeza umaskini kwa mtu mmoja mmoja, akisisitiza kuwa ahadi za maendeleo kama maji na barabara zitafanyika endapo tu nchi itakuwa na amani



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...