Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Nyumba mpya ya watoto Yatima iliyopo Mazizini nje ya Mji wa Zanzibar,awali nyumba hiyo ya watoto yatima ilikuwepo Forodhani MjiMkongwe wa Zanzibar,(kulia)Mke wa Rais Mama Shadya Karume,mwenyekiti wa Jumuiya inayoshuhulikia mazingira na maendeleo ya vijana,ZAYEDESA.
CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO
Chama cha Kulinda na Kuwatetea Walimu Tanzania (CHAKUWAHATA) kimemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuingilia kati sakata la baadhi ya wakurugenzi kukiuka sheria ya kuwaruhusu walimu kujiunga na chama hicho hivyo makato ya fedha za mishahara yao kuingizwa kwenye chama hicho. Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Emmanuel Herman alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari wakati wa Mkutano Mkuu wao unaofanyika jijini Dodoma. Walimu ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kupitia upya rasimu ya katiba ili ieendane na wakati.
Comments