4x4

KIKAO CHA WACHEZAJI WA ZAMANI LEO UWANJA WA TAIFA


Aliyekuwa mgombea Urais katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ally Mayay akitoa shukrani zake kwa wachezaji wenzake wa zamani nchini katika kikao kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Mchezaji wa zamani wa Tukuyu Stars, Simba na Yanga, Suleiman Mathew (kushoto) akiwa na kiungo wa zamani wa Yanga, Thabit Badru Bushako 
Kutoka kushoto Ngade Chabanga, Abubakar Mtiro na Juma Pinto
Wachezaji wa zamani wa Simba, Spear Mbwembwe (kulia) na George Masatu (kushoto)
Wachezaji wa zamani wa Simba, Mashaka Ayoub (kushoto) na Said Maulid 'SMG' (kulia) aliyecheza na Yanga pia
Wachezaji wa zamani wa Yanga, Manyika Peter (kushoto) na Shaaban Ramadhan aliyecheza na Simba pia 
Kiongozi Mkuu wa umoja huo unaojulikana na kama Galactico, Muddy Sebene (kushoto) akiwa na kiungo wa zamani wa Yanga, Mohammed 'Rishard' Adolph 
Wachezaji wa zamani wa Simba, Madaraka Selemani (kulia), Duwa Said (kushoto) na George Lucas 'Gazza' nyuma yao
Richard Mwaikenda

Posted in

Spread the love

NYAMLANI, MGOYI WAULA KAMATI YA UTENDAJI TFF, KIDAU KATIBU MKUU


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amewateua Makamu wa Rais wa zamani wa TFF, Athuman Nyamlani na Ahmed Mgoyi kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
Rais Karia ameteua kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo katika Katiba ya TFF ikiwa ni wiki moja baada ya kupatikana kwa viongozi wa shirikisho katika uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 12, mwaka huu.
Rais Karia aliwatambulisha viongozi hao kwenye Kikao cha Kamati ya Utendaji iliyofanyika Jumanne Agosti 22, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kamati ya Utendaji ya TFF PIA imepitisha jina la Kidao Wilfred kuwa Kaimu Katibu Mkuu.
Kidao ambaye ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars ambaye pia Mwenyekiti wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA), ameteuliwa rasmi jana Agosti 22, 2017 na Kamati ya Utendaji ya TFF. Wasifu wa Kidao utawajia punde.
Katika kikao hicho pia Rais Karia alitumia fursa hiyo kutangaza viongozi wa kamati mbalimbali za TFF zikiwamo za kinidhamu na kisheria.
Kamati ya Nidhamu: Mwenyekiti Tarimba Abbas, Makamu Mwenyekiti, Peter Hella wakati wajumbe ni Boniface Lyamwike, Dk. Bill Haonga na Kassim Dau.
Kamati ya Rufani za Nidhamu: Mwenyekiti ni Wakili Rahim Zuber Shaban; Makamu Mwenyekiti, Stella Mwakingwe wakati Wajumbe ni Abbas Mtemvu, Amani Mulika na Siza Chenja.
Kamati ya Maadili: Mwenyekiti ni Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu Mwenyekiti ni Wakili Steven Zangira wakati Wajumbe ni Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.
Kamati ya Rufaa ya Maadili: Mwenyekiti ni Wakili Ebenezer Mshana; Makamu Mwenyekiti ni DCP. Mohammed Mpinga na wajumbe  ni Wakili Benjamin Karume, George Mayawa na ASP. Benedict Nyagabona.
Kamati ya Uchaguzi: Mwenyekiti ni Revocatus Kuuli; Makamu Mwenyekiti ni Wakili Mohammed Mchengerwa; Wakili Edwin Mgendera; Wakili Kiomoni Kibamba na Wakili Thadeus Karua.
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi: Mwenyekiti ni Kenneth Mwenda; Makamu Mwenyekiti ni Jabir Shekimweri na Wajumbe ni Wakili Rashid Sadalla, Irene Kadushi na Mohammed Gombati.
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji: Mwenyekiti ni Elias Mwanjala; Makamu Mwenyekiti ni Wakili Malangwe Mchungahela wakati Wajumbe ni Zakaria Hanspope, Robert Selasela, Goodluck Moshi, Mhandisi Issa Batenga na Hamis Semka.
Kamati ya Fedha na Mipango: Mwenyekiti ni Michael Wambura; Makamu Mwenyekiti ni Francis Ndulane na Wajumbe ni Almas Kasongo, Pascal Kihanga, Maximillian Tabonwa, Paul Bilabaye na Farid Abeid.
Kamati ya Mashindano: Mwenyekiti ni Ahmed Mgoyi; Makamu Mwenyekiti ni James Mhagama wakati Wajumbe ni Kenneth Pesambili, Shafii Dauda, Fortunatus Kalewa na Mhandisi Andrew Makota.
Kamati ya Ufundi: Mwenyekiti ni Vedastus Lufano; Makamu Mwenyekiti ni Issa Bukuku na wajumbe ni Sarah Chao, Ally Mayay, Michael Bundala, Omar Abdulkadir na Israel Mujuni.
Kamati ya Soka la Vijana: Mwenyekiti ni Khalid Abdallah; Makamu Mwenyekiti ni Lameck Nyambaya na Wajumbe ni Mohammed Aden, Ramadhani Nassib, Salim Kibwana na Vicent Majili.
Kamati ya Mpira wa Wanawake: Mwenyekiti ni Amina Karuma; Makamu Mwenyekiti ni Rose Kissiwa na Katibu wa Kamati hiyo ni Somoe Ng’itu wakati Wajumbe ni Zena Chande, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Zuhura Kapama na Nia Mjengwa.
Kamati ya Waamuzi: Mwenyekiti ni Saloum Chama; Makamu Mwenyekiti Joseph Mapunda wakati Wajumbe ni Nassib Mabrouk, Leslie Liunda na Soud Abdi.
Kamati ya Habari na Masoko: Mwenyekiti ni Dunstan Mkundi; Makamu Mwenyekiti ni Mbasha Matutu wakati Wajumbe ni Imani Kajura, Mgaya Kingoba, Godfrey Dilunga na Samson Mbamba.
Kamati ya Ukaguzi wa Fedha: Mwenyekiti ni Yahya Hamad; Makamu Mwenyekiti ni Athuman Nyamlani na Wajumbe ni Khalifa Mgonja, Japhary Kachenje, Jackson Songoro na Benesta Rugora.
Kamati ya Tiba: Mwenyekiti ni Dkt. Paulo Marealle; Makamu Mwenyekiti ni Dkt. Fred Limbanga Wakati wajumbe ni Dkt. Norman Sabun, Dkt. Lisobina Kisongo, Dkt. Eliezer Ndalama, Dkt. Elson Maeja na Violet Lupondo.
Kamati ya Futsal na Beach Soccer: Mwenyekiti ni Ahmed Mgoyi; Makamu Mwenyekiti ni Hussein Mwamba na Wajumbe ni Blassy Kiondo, Isaac Munisi, Didas Zimbihile na Aaron Nyanda.
Kamati ya Ajira: Mwenyekiti ni Issa Bukuku; Makamu Mwenyekiti ni Saloum Chama wakati Wajumbe ni Athuman Kihamia, Mtemi Ramadhani, Noel Kazimoto na Hawa Mniga.
Kamati ya Leseni za Klabu: Mwenyekiti ni Wakili Lloyd Nchunga; Makamu Mwenyekiti Wakili Emmanuel Matondo wakati Wajumbe ni Profesa Mshindo Msolla, Hamisi Kissiwa na David Kivembele.
Kamati ya Rufaa za Leseni: Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro; Makamu Mwenyekiti ni Wakili Alex Mngongolwa Wajumbe ni Meneja wa zamani wa Uwanja wa Taifa, Charles Matoke, Tumainiel Mlango na Ahmed Menye.
Richard Mwaikenda

Posted in

Spread the love

YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI LEO July August 23, 2017.

Richard Mwaikenda

Posted in

Spread the love

YANGA YAWAPIGA CHENGA WACHAWI WA SIMBA AIRPORT DAR.

TIMU ya Yanga imetua Uwanja wa Ndege wa zamani Dar es Salaam kwa kuwapiga chenga ya mwili 'wachawi' wa Simba.

Yanga waliowasili saa 12:30 jana jioni kwa Ndege ya kukodi kutoka Pemba, wakiongozwa na Mama Fatma Karume walikwepa kupita mlango wa kawaida wa abiria ambako inadaiwa 'wachawi' wa Simba waliojichanganya na mashabiki walikuwa wanawasubiri ili wawatende.

Kwa mujibu wa Mmoja wa wafanyakazi wa Ndege za kukodi aliyekuwepo uwanjani, alishuhudia Timu hiyo ikikwepa mtego huo kwa kupanda kwenye coaster iliyoingizwa ndani mapema ikitoka Aiport kupitia geti la Polisi na kutokomea town.

Kitendo hicho kiliwaacha hoi 'wachawi. hao pamoja na Mashabiki wa Yanga waliobaki kulikodolea macho gari hilo likitokomea.

Shuhuda huyo anasema kuwa 'wachawi' wa Simba waliokuwepo hapo walionekana kupigwa na mshangao huku wakiwa wameshika mikono kichwani na kusikika wakisema "Ayaa wamepitia kule sasa tumekwisha."

Alisema kuwa makomandoo wa Yanga walikuwepo uwanjani hapo tangu mapema kuweka usalama kwa timu yao ili isidhurike kwa lolote ambapo walionekana kuwapiga mkwara mzito waliowahisi kuwa 'Wachawi' wa Simba kwa kuwaamuru kuondoka na kuacha kukaribia lango la kutokea abiria.

Timu hiyo inayocheza na Simba  kwenye Ngao ya Jamii ilipokelewa Airport na Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa na Shadrack  Nsajigwa.
Richard Mwaikenda

Posted in

Spread the love

SHUGHULI PEVU SIMBA NA YANGA TAIFA LEO...LWANDAMINA KUENDELEZA UNYONGE KWA OMOG?

Na mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM

KOCHA Mzambia wa Yanga, George Lwandamina leo ataiongoza timu hiyo katika mchezo wa tatu dhidi ya Simba, akiwa na rekodi ya kufungwa mechi zote mbili zilizotangulia.
Yanga inakutana na mahasimu wao wa jadi, Simba katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii kuanzia Saa 11:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuashiria ufunguzi rasmi wa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Huo utakuwa mchezo wa tatu kwa Mzambia, George Lwandamina tangu achukue nafasi ya Mholanzi, Hans van der Pluijm Desemba mwaka jana na mechi mbili zilizopita zote alipoteza.  
Januari 10, mwaka huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar – Yanga ilifungwa kwa penalti 4-2 na Simba baada ya sare ya 0-0 katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Na Februari 26, mwaka huu, Simba ikatoka nyuma na kushinda 2-1 kwa mabao ya Mrundi Laudit Mavugo dakika ya 66 na mzawa, Shiza Kichuya dakika ya 81, baada ya Simon Msuva kuanza kuifungia Yanga kwa penalti dakika ya tano.
Kocha Mzambia, George Lwandamina amefunga mechi zote mbili alizokutana na Simba chini ya kocha Mcameroon, Joseph Omog

Na mechi zote Lwandamina amefungwa na Simba ikiwa chini ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog akisaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja ambao wote leo watakuwepo kwenye benchi la Simba kama kawaida.
Katika benchi la Yanga kuna mabadiliko kidogo, kocha msaidizi wa msimu uliopita, Juma Mwambusi hayupo na nafasi yake imechukuliwa na beki na Nahodha wa zamani wa timu hiyo, Nsajigwa Shadrack Joel Mwandemele. 
Kwenye benchi la Simba, ameondoka kocha wa makipa Mkenya, Iddi Salim na nafasi yake kuchukuliwa na golikipa wa zamani wa timu hiyo, Muharami Mohammed ‘Shilton’.
Kiungo Haruna Niyonzima leo ataibukia kwa mahasimu Simba, baada ya miaka sita ya kucheza Yanga tangu alipojiunga nayo mwaka 2012 akitokea APR ya kwao, Rwanda. Yanga pia imempoteza mchezaji wake mahiri na aliyekuwa tegemeo katika safu ya ushambuliaji, Simon Msuva aliyehamia Difaa Hassan El- Jadida ya Ligi Kuu ya Morocco.
Mshambuliaji Ibrahim Hajib naye leo ataibukia kwa watani, Yanga baada ya kuibukia timu ya vijana ya Simba na kupandishwa kikosi cha kwanza cha timu hiyo alikopatia umaarufu. Simba pia haitakuwa na beki wake, Abdi Banda aliyehamia Baroka FC ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Lakini timu zote zimejiimarisha kwa usajili mzuri wa wachezaji wapya, wanaotarajiwa kuchukua nafasi leo kama Aishi Manula, Said Mohammed, Erasto Nyoni, Ally Shomary, Salim Mbonde, Jamal Mwambeleko, Yussuf Mlipili, Paul Bundala, Shomary Kapombe, John Bocco, Nicholas Gyan na Emmanuel Okwi kwa upande wa Simba na Youthe Rostand, Ramadhan Kabwili, Gardiel Michael, Abdallah Haji ‘Ninja’, Papy Kabamba Tshishimbi, Raphael Daudi, Pius Buswita na Baruan Akilimali kwa Yanga. 
Timu zote zilikuwa kambini upande wa pili wa Muungano wa Tanzania kwa wiki nzima – Yanga walikuwa kisiwani Pemba na Simba walikuwa Unguja na kabla ya mchezo wa leo, kila timu imecheza mechi sita za kujipima na kila moja ilipoteza mchezo mmoja.
Simba ilifungwa 1-0 na Orlando Pirates, kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Bidvest Wits nchini Afrika Kusini, ikashinda 1-0 na Rayon Sport ya Rwanda, 1-0 na Mtibwa Sugar, 0-0 na Mlandege na kumalizia kwa ushindi wa 5-0 dhidi ya Gulioni FC, wakati Yanga ilishinda 5-0 na Moro Kids, 3-2 na Singida United, ikafungwa 1-0 na Ruvu Shooting, ikashinda 2-0 na Mlandege, 1-0 na Chipukizi na 1-0 na Jamhuri.    
Kwa ujumla makocha wote wana changamoto ya kuviunganisha vikosi vyao baada ya usajili wa wachezaji wapya wengi ili kutengeneza uwiano mzuri wa timu iweze pia kucheza kwa uelewano.
Mara ya mwisho Yanga kuifunga Simba ilikuwa ni Februari 20, mwaka 2016 ushindi wa 2-0 uliotokana na mabao ya mshambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma dakika ya 39 na Amissi Tambwe dakika ya 72, ambao kwa pamoja leo wanatarajiwa kuiongoza tena timu hiyo.
Lwandamina atafuta uteja kwa Simba leo? Hilo ndilo swali na majibu yatapatikana baada ya mchezo. 

KWA HISANI YA BIN ZUBEIRY ONLINE
Richard Mwaikenda

Posted in

Spread the love

MAGAZETI YA TZ NA NJE LEO AUG 23,2017Richard Mwaikenda

Posted in

Spread the love