DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akishiriki utoaji wa heshima za mwisho, kumwaga mchanga na kuweka shada la maua, wakati wa mazishi ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Jimbo la Mara Kaskazini, marehemu Fransisca Mwita Gachuma, yaliyofanyika Jumamosi, Machi 30, 2024, huko Komaswa, Tarime Vijijini. Askofu Gachuma alikuwa mwenza wa Ndugu Christopher Mwita Gachuma, ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, kutokea Mkoa wa Mara.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana na kuzungumza jambo na Askofu Mkuu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Dkt. Daniel Ouma (mwenye joho), mara baada ya misa ya kumuombea marehemu, 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Ndugu Kassim Majaliwa Majaliwa, alipowasili kushiriki shughuli ya mazishi ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NGLCC), Jimbo la Mara Kaskazini, Fransisca Mwita Gachuma, 

Sehemu ya umati wa waombolezaji wakishiriki misa ya kumuombea marehemu, wakati wa mazishi ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Jimbo la Mara Kaskazini, Fransisca Mwita Gachuma, Jumamosi, Machi 30, 2024, huko Komaswa, Tarime vijijini, mkoani Mara. Askofu Gachuma alikuwa mwenza wa Ndugu Christopher Mwita Gachuma, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) Taifa, kutokea Mkoa wa Mara.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI