Mtoto Bwaga Abdallah akipokea mfuko wa sukari kutoka kwa maofisa wa Vodacom Foundation, Grace Lyon (kulia) na Mwamvua Mlangwa (wa pili kutoka kulia) huku akisaidiwa na Sheikh Mohamed Khalili (kushoto) kutoka Tanga mjini na Sheikh Khamis Rashid Mwakilishi wa Sheikh wa Pangani (wa pili kutoka kushoto). Katika hafla hiyo iliyofanyika juzi mjini Pangani, Tanga, Vodacom Foundation pamoja na kufuturisha ilitoa pia msaada wa mchele, maharage, mafuta ya kula na vifaa vya shule.
CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO
Chama cha Kulinda na Kuwatetea Walimu Tanzania (CHAKUWAHATA) kimemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuingilia kati sakata la baadhi ya wakurugenzi kukiuka sheria ya kuwaruhusu walimu kujiunga na chama hicho hivyo makato ya fedha za mishahara yao kuingizwa kwenye chama hicho. Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Emmanuel Herman alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari wakati wa Mkutano Mkuu wao unaofanyika jijini Dodoma. Walimu ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho wakiwa katika mkutano wa kupitia upya rasimu ya katiba ili ieendane na wakati.
Comments