VODACOM YATOA MSAADA WA MAGODORO, MABRANKETI NA VYAKULA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR

Baadhi ya watoto walioathirika kwa mafuriko, wakisaidia kubeba magodoro yaliyotolewa msaada na Kampuni ya Vodacom Tanzania, kwa walioathirika katika Kambi iliyopo Shule ya Msingi Mchikichini, Dar es Salaam jana. Vodacom ilitoa msaada wa magodoro 430, mabranketi 800 na vyakula, vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 30. (
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom wakiwa na magodoro wakiyapeleka sehemu ya kuyahifadhi
Wafanyakazi wa Vodacom wakipakua magodoro kwenye magari
Meneja wa Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akizungmza baada ya kukabidhi msaada huo
Baadhi ya Wafanyakazi wa Vodacom wakisaidia kuanika nguo za waathirika wa mafuriko


* Yatoa magodoro, mablanketi na vyakula kwenye kambi
Dar es salaam Disemba 23, 2011. Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom leo imekabidhi msaada wenye thamani ya shilingi 30 Milioni kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam wanaoishi katika makambi maalum yaliyofunguliwa kuwawezesha kujihifadhi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya.

Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule amekabidhi msaada huo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Sadik Meck Sadiq ukijumuisha magodoro 430 mablanket 800,na vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni kumi.

"Tumeshtushwa sana na hali halisi ya maafa yaliyotukumba jijini Dra es salaam, tumefika hapa kuendeleza utamaduni wa Vodacom kwa kuonesha upendo na kuwa karibu na wananchi katika nyakati za raha na shida."Alisema Mwakifulefule.

Vodacom imekabidhi msaada huo kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ambao umekuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za maendeleo katika jamii na pia kufariji waathirika nyakati za maafa.

"Mafuriko haya yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi kuwahi kutokea Dar es salaam katika muda wa miaka mingi iliyopita na hivyo ni wazi athari zake ni kubwa, tunatoa pole kwa wote waliopoteza watoto, ndugu na jamaa na wale walionusurika tunawatakia afya njema na faraja katika wakati huu mgumu wa maisha wanaoupitia"Aliongeza Mwakifulefule Adha kampuni hiyo imetangaza pia fursa kwa wateja wake na wa wananchi kwa ujumla kuungana na Menejimenti na wafanyakazi wake kuchangia walichonacho kupitia nambari maalum ya maafa ya Vodacom Red Alert na kwa njia ya m-pesa.

Kupitia nambari ya Red Alert wananchi wanaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi - SMS wenye neno "MAAFA" kwenda nambari15599 na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.

"Mahitaji kwa wenzetu waliothirika ni makubwa. Tuna imani kuwa wote kwa pamoja tutaonesha umoja, upendo na mshikamano wetu wa kitaifa unaojenga tunu ya Utanzania wetu kusaidia wenzetu ambao kwa wakati huu wapo katika mashaka makubwa wakihitaji faraja ya kila aina". Amesema Mwakifulefule.

Michango yote itakayokusanywa kupitia nambari hizi itawasilishwa kwa kamati ya Maafa ya mkoa kuongeza nguvu katika juhudi za kuwasaidia waathirika na kwamba utaratibu wa kuwapatia taarifa wachangiaji utakuwepo.

Aidha kampuni ya Vodacom Tanzania imevipongeza kipekee vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa juhudi kubwa za uokozi kwa kushirikiana na wananchi hatua ambayo imesaidia kunusuru maisha ya maelfu ya watu.

Jinsi ya kuchangia kwa m-pesa
*150*00# kupata orodha ya huduma za m-pesa.
Hatua ya 2: Chagua 4 - Lipa Bili
Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni - weka namba 155990 Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu - weka namba yako ya simu Hatua ya 5: Weka kiasi - ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri Hatua ya 7:Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia.

Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA

NOTI MPYA KUANZA KUSAMBAZWA MWEZI UJAO