UZINDUZI WA SKAUTI KUFANYIKA FEBRUARI 25 MWAKA HUU

Uzinduzi wa kumbu kumbu ya mwanzilishi wa skauti Ulimwenguni bw Robert Baden PowelL na mkewe Bi. Oliva Powell(lady baden powell)kimkoa umefanyika leo na kilele ni siku ya tar.25 ya mwenzi huu kwenye viwanja vya sheikh Amri Abeid jijini hapa kwa maonyesho na matamasha kote nchini.

Hayo yamesemwa nakamishina mkufunzi mkuu wa taifa bi Margareth Olumbe wakati akisoma risala ya maskauti wa kike hapa Arusha na kusema kuwa girl guide hapa nchini ilanzishwa mnamo mwaka 1928 na girl guide 9 na walijiita 1st Kilimanjaro na walikuwa na uhusiano na mke wa gavana wa wakati huo ukaingia ukimya wa muda mrefu na guiding haikusikika hadi 1934 mke wa gavana Lady Mack alianzisha kampuni nyingine Dar es-salaam na ikaitwa 1st Dar –es-salaam kampuni na ilikuwa na wazungu tu baadae alianzisha first dar-es-salaam Brownes na ilkuwa mchanganyiko.

Kuna changamoto nyIngi kubwa zinazowakabili girl guide hapa mkoani na taifa kwa ujumla zikiwemo kuwatoa watoto katika tabia hatarishi kuwa raia wema,wazazi ambao wangesaidiana nasi wamekuwa na shughuli nyingi na wengine hawafikiki hata na watoto wao,mwitiko wa wananchi

Akatoa ombi kwa mgeni rasmi ambaye alimwakilisha mlezi wa skauti wa kike hapa nchini mama Salma Kikwete bi Pendo Laizer kutoka(CASEC) kuwa awe mlezi wa girl guide wa arusha na mgeni huyo kukubali kuwa mlezi na kuwatafutia wafadhli wakukisaidia girl guide mgeni huyo aliambatana na mgeni kutoka nchini uingereza bi jill Nicholson na Yona .M.Mziba kutoka kitengo cha polisi jamii mkoani hapa.Chanzo;Full Shangwe

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*