Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akisaidia kusomba matofali ya kujengea nyumba ya Balozi wa Shina la CCM namba 12, la Isenge katika Kata ya Dutwa alipokuwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama pamoja na kukagua mIradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa Ilani ya CCM, katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
|
Katibu wa CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto0 na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), wakisaidiana na wanachama wa wengine wa CCM kuchimba msingi wa nyumba ya Balozi wa Shina namba 12 la Isenge katika Kata ya Dutwa, Jimbo la Bariadi Magharibi leo. |
Wanachama wa CCM wakisaidia kuchimba msingi wa ujenzi wa nyumba ya Balozi wa shina namba 12 la Isenge, wilayani Bariadi.
|
Kinana akisalimiana na ofisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) wilayani Bariadi |
Kinana akizungumza na wanachama wa CCM wa Tawi la Isenge,katika Kata ya Dutwa Bariadi
|
Kinana akimpatia Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi , Andrew Chenge ili azungumze katika mkutano huo |
Kinana akishiriki kula chakula cha asili aina ya mchembe ambacho ni viazi vilivyokaushwa
|
Nape alkila wali kwa maharage pamoja na wananchi chakula kilichoandaliwa na Balozi kwa ugeni huo |
Wananchi wa Kijiji cha Yoma, Kata ya Somanda wilayani Bariadi, wakishangilia kuonana na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana ii asuhishe mgogoro maji ktika kijiji hicho.
|
Wananchi wakitoa malalamiko yao kwa Kinana na kumuomba auamuru uongozi akiwemo mhandisi wa maji wa wilaya ya Bariadi, kuwapatia haraka maji kutoka kwenye kisima kilichopo katika kijiji hicho. |
|
Kinana akiwasihi wananchi hao kuwa wavumilivu hadi Oktoba muda ambao wameahidiwa na uongozi kuwa wataanza kupata maji. |
Kinana akisaidia kujnga vyoo vya Shule ya Sekondari ya Malambo, Bariadi mjini leo
|
Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge akiahidi kujenga moja ya vyumba vya madarasa katika shule ya Malambo |
|
Chenge akielezea katika mkutano wa hadhara ahadi mbalimbali zilizotekelezwa na yeye pamoja na serikali katika jimbo hilo |
|
Nape akihutubia mkutano wa hadhara mjini Bariadi,mbapo pamoja na mambo mengine aliwashambulia viongozi wa chadema kuhusu kitendo cha kumwandama Balozi wa China nchini, Lu Youqing ambaye amewezesha viwanda kumi vya nguo, mafuta na nyama kujengwa mkoani Shinyanga pamoja na kujenga chuo cha kuboresha zao la pamba. Viwanda hivyo vitakuwa na uwezo wa kuajiri vijana zaidi ya 20,000. PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG |
Kinana akihutubia wananchini katika mkutano wa hadhara mjini Bariadi, ambapo pamoja na mambo mengine, aliwataka viongozi wanaowatesa waalimu kwa kutowatekelezea maslahi yao, wajuzulu mara moja.
|
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wa hadhara |
Kinana akimkabidhi pikipiki mmoja wa viongozi wa bodaboda zilizotolewa na baadhi ya viongozi wa ccm wialyani humo
|
Kiongozi wa Bodaboda wilayani Baraiadi, Masumbuko Nchina akiapatiwa na Kinana sh.mil. 1 iliyotolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Simiyu, Njalu Silanga |
Momoja wa wanachama wapya wa CCM, akipatiwa na Kinana kadi yake ya uanachama katika mkutano huo wa hadhara
Comments