MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA NYUMBA 851 ZA WATUMISHI WA UMMA ENEO LA BUNJU 'B' WILAYA YA KINONDONO MKOA WA DAR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Nyumba 851 za Watumishi wa Umma
zinazojengwa katika eneo la Bunju B, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es
Salaam, wakati wa sherehe hiyo liyofanyika leo. Kutoka (kushoto) ni Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya kudumu ya Miundombinu, Peter Serukamba, Waziri wa Ujnezi, Dkt. John
Pombe Magufuli na (kushoto) kwa Makamu ni Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius
Mwakalinga na Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi. Picha zote na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa moja kati ya Nyumba 851, baada
ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba hizo za Watumishi wa Umma
zinazojengwa katika eneo la Bunju B, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es
Salaam, wakati wa sherehe hiyo liyofanyika leo. Kushoto ni Mtendaji Mkuu
wa TBA, Elius Mwakalinga na (kulia) ni Waziri wa Ujnezi, Dkt. John
Pombe Magufuli.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwahutubia wananchi wa Bunju B, wakati alipofika kuweka Jiwe la
Msingi la Ujenzi wa Nyumba 851 za Watumishi wa Umma zinazojengwa katika
eneo hilo, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, wakati wa sherehe
hiyo liyofanyika leo. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Comments