MFUKO WA BIMA YA AFYA IRINGA NA NJOMBE WAONYA VITUO VYA AFYA VINAVYOWANYIMA DAWA WATEJA
Bw Deusdedit G. Rutazaa kutoka mfuko wa bima ya afya Taifa akizungumza na wanahabari leo kuhusu kongamano la wadau wa mfuko wa bima ya afya litakalofanyika kesho mjini Iringa |
Wateja wakipata huduma ya bure ya upimaji wa kisukari leo mjini |
wateja wakipata wakisubiri kupata huduma ya bure leo |
Wateja wakifurahia huduma ya bure leo mjini Iringa katika maandalizi ya mkutano mkuu wa wadau wa bima ya afya |
Wateja wakifurahia huduma ya bima ya afya |
Wananchi Iringa wakiwa katika foleni ya kupima afya zao bure leo mjini Iringa |
kauli hiyo imetolewa leo mjini Iringa wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa bure wa magonjwa ya kisukari bure kwa wakazi wa mji wa Iringa kama sehemu ya maandalizi ya mkutano mkuu wa wadau kwa mkoa wa Iringa na Njombe .
Akizungumza kwa niaba ya kaimu mkurugenzi mkuu wa mfuko wa bima ya afya Bw Deusdedit G. Rutazaa alisema kuwa mbali ya mfuko huo kufikiwa na mafanikio makubwa kwa kuwa na wateja wengi zaidi ila wapo baadhi ya wato huduma katika vituo vya afya ,maduka ya madawa na Hospital ambao wameendelea kuwasumbua wateja wa mfuko wa bima ya afya jambo ambalo dawa yake ipo jikoni .
Rutazaa alisema kuwa lengo la mkutano mkuu wa wadau kufanyika mkoani Iringa ni kutaka kupokea changamoto mbali mbali ambazo wateja wamekuwa wakikumbana nazo ,mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa St Dominic kesho jumatatu .
Hata hivyo alisema kwa mkoa wa Iringa wameanza mandalizi ya mkutano huo leo kwa kutoa huduma za bure za upimaji wa shinikizo la damu ,kisukari pamoja na kutoa ushauri kwa wananchi katika kuboresha afya zao.
Rutazaa alisema kuwa toka mfuko huo kuanzishwa mkoa wa Iringa kumekuwepo na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa wanachama na kuboresha zaidi huduma za afya .
Pia alisema mfuko huo umesajili vituo vya afya kama maduka ya madawa ili kuwawezesha wateja kupatiwa huduma kwa ufanisi zaidi .
Comments