RC ISHENGOMA AZIBANA HALMASHAURI IRINGA KUWASILISHA MFUKO WA BIMA YA AFYA KIASI CHA TSH MILIONI 87 ZA TELE KWA TELE
viongozi mbali mbali na wadau wakiwa katika mkutano huo leo katika ukumbi wa St Dominic |
Viongozi wa kitaifa na mkoa wa Iringa waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mfuko wa bima ya afya mkoa wa Iringa leo |
Wafanyakazi wa mfuko wa bima ya afya Taifa na mkoa wa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa mfuko huo na serikali ya mkoa wa Iringa leo |
.............................................................................................................................................
MKUU
wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma amezitaka Halmashauri
za wilaya katika mkoa wa Iringa ambazo hazijawasilisha madai ya
tele kwa tele yenye jumla ya shilingi milioni 87 kwa ajili ya
mfuko wa bima ya afya kuwasilisha mara moja.
Pamoja
na kuzitaka halmashauri hizo kuwasilisha fedha hizo pia mkuu
huyo wa mkoa alitangaza kuwachukulia hatua kali watoa huduma
katika vituo vya afya ambao wanahujumu mfuko huo wa bima ya afya
kwa kughushi huduma za matibabu za mfuko huo na mingine ya afya.
Mkuu
huyo wa mkoa alitoa agizo hilo leo wakati akifungua mkutano
wa siku ya wadau wa mfuko wa bima ya afya mkoa wa Iringa ,uliofanyika
katika ukumbi wa St Dominic mjini Iringa .
Alisema
kuwa zipo changamoto ambazo serikali ya mkoa wa Iringa imepata
kuziona ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ikiwemo changamoto ya
uchakavu wa baadhi ya vituo vya serikali kama vile Zahanati ya
Isele, Ilolompya,Mapogoro ,Kising'a na Mtandika pamoja na upungufu wa
dawa hasa katika vituo vya serikali .
Dr
Ishengoma alisema kuwa serikali imejipanga kufanyia kazi
changamoto hizo japo alisema hali ya uandikishaji wanachama wapya
wa mifuko hiyo katika mkoa bado si ya kuridhisha mbali ya kuwa
mkoa wa Iringa unaongoza kwa kuandikisha wanachama wengi katika
Tanzania kwa kuwa nafasi ya nne kutimiza lengo la kuandikisha kaya
12,244 hadi juni 30 mwaka huu ambayo ni sawa na asilimia 9.6 ya
malengo ya kuandikisha kaya 127,561 ifikapo mwaka 2014/15 .
Pia
aliwataka watoa huduma kuhakikisha wanawapa huduma wanachama wa
NHIF na CHF sawa na wananchi wengine bila ya ubaguzi wowote kwa
kuwa mojawapo ya malalamiko yanayotokana na wanachama wa mifuko hiyo
ni pamoja na kubaguliwa katika huduma kwa kuonekana kama watu
wanaotibiwa bure mtazamo ambao si sahihi kwa maana gharama za
matibabu kwa wanachama hao tayari zimelipwa kupitia mifuko hiyo.
"
Nawaagiza watoa huduma wote kuacha mara moja tabia hiyo
isiyozingatia utu ....watakaobainika kuwasumbua wagonjwa ambao ni
wanachama wa mifuko hiyo tutawachukulia hatua kali zaidi "alisema
mkuu huyo wa mkoa
Katika
hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa aliwataka wanachama wa mifuko
hiyo ya NHIF na CHF kuendelea kutumia kadi zao halali na kuachana
na mpango wa kuazimishana kadi za matibabu ama kufanya biashara kwa
kutumia kadi hiyo kwa ajili ya kughushi huduma za matibabu .
Kwa
upande wake mwenyekiti wa bodi ya NHIF balozi Ali Mchumo(pichani juu) alisema
kuwa katika kuhamasisha wananchi wengi zaidi kuendelea kujiunga
na mifuko hiyo unaanzishwa utaratibu wa kutoa tuzo ya bima ya afya
kwa wote kwa wilaya ambazo zitafanya vema katika kuingiza idadi
kubwa zaidi ya wanachama.
Alisema
kuwa lengo la serikali ni kuona watanzania wote wanapata huduma
bora ya afya kwa kujiunga na mifuko hiyo hivyo ili kutimiza
lengo hilo ni lazima kila kiongozi na kila wilaya kufanya
uhamasishaji ili kila mtanzania kujiunga na mifuko hiyo.
Comments