MBUNGE FILIKUNJOMBE ATIMIZA AHADI ZAKE KWA KANISA LA ANGLIKANA ILELA LUDEWA

Waumini  wa Kanisa la  Anglikana  Ilela  Ludewa  wakimshangilia  mbunge  wao  Deo  Filikunjombe  wakati  akitolea ufafanuzi  wa misaada  anayoitoa  kanisani hapo  ,wakati  wa ibada ya Krismas
Mmoja kati ya  waumini wa kanisa  hilo akishukuru kwa  kulala  chini  wakati  mbunge  wao akitoa  misada  yake
Mbunge  wa   jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe wa pili  kulia akikabidhi msaada wa marumaru  seti  100 kwa  mchungaji wa kanisa la  Anglikana mtaa  wa  Ilele  Ludewa mchungaji Canon Ngoye
Wananchi  na  waumini  wa kanisa la Anglikana   mtaa wa Ilela  Ludewa  wakimuwekea mikono ya baraka  mbunge Deo Filikujombe baada ya  kukabidhi misaada kanisan i hapo
Waumini  wa kanisa la Anglikana  mtaa wa Ilela Ludewa akifurahi pamoja na mke  wa mbunge Deo Filikunjombe Bi Habiba Filikujombe mwenye nguo  nyekundu kati
Waumini  wa kanisa  hilo  wakimshangilia mbunge  wao
Mmoja  kati  ya  waumini  wa kanisa  hilo  akimfuta jasho mbunge  Deo Filikunjombe kama  ahsante kwa  kuwajali  wapiga kura  wake
Mbunge  Filikunjombe  akitoa neno kwa  wapiga kura  wake kanisani  hapo
Mbunge  Deo Filikunjombe  akitoa  neno
Mkuu  wa wilaya ya  Ludewa  Juma  Madaha  kulia akiwa na mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kati  na mwenyekiti  wa CCM wilaya ya  Ludewa Bw  Kolimba  wakati  wa ibada ya Krismas jana
 Mchungaji  wa kanisa  la Anglikana  mtaa wa Ilela  Canon Ngoye  akikabidhiwa  kinada na  mbunge Deo Filikunjombe
 Mchungaji  Ngoye  akikabidhiwa  saruji mifuko  20 kutoka kwa  mbunge  Deo Filikunjombe  wakati wa ibada ya Krismas
 ..........................................................................................................................................
MBUNGE   wa  jimbo  la Ludewa  mkoani Njombe  Deo  Filikunjombe  amekabidhi  msaada  wa  vitu  mbali mbali  kwa uongozi  wa kanisa  la  Angilikana  mtaa  wa Ilela  wilaya  ya   Ludewa kama  sehemu  ya  kutimiza ahadi  yake  kwa  waumini  wa  kanisa  hilo.

Mbunge  huyo  alitimiza ahadi hiyo   wakati  wa  idaba ya  Krismas  ambapo  alijumuika na  familia  yake  kusali pamoja na  kula  na  wagonjwa  wa kituo cha afya Manda   kama sehemu  ya  mwendelezo  wa  ushirikiano  wake  na  wapiga kura  wake  .

Alisema  kuwa  kila  sikukuu  amekuwa na  utamaduni  wa  kuzunguka katika moja kati ya  kanisa  la jimboni kwake na  kula sikuku ya  wagonjwa  pamoja na  kusali  na  waumini  wa  madhehebu  mbali mbali jimboni  humo lengo likiwa ni kuhimiza  shughuli za maendeleo  jimboni .

 Hata   hivyo  akizungumzia mambo mbali mbali ya  kimaendeleo katika  jimbo  hilo alisema  kuwa  ameendelea   kuisukuma  serikali  kutatua  kero  za wananchi  wa  jimbo la  Ludewa ikiwa  ni  pamoja na kuboresha  miundo mbinu ikiwemo barabara  , afya  ,elimu  ,maji  na kero nyingine  ambazo wananchi  wamekuwa  wakihitahi  ufumbuzi  wake.

Filikunjombe  alisema  kuwa kuhusu  kilichotokea  bungeni  kwa  mawaziri wanne  kuenguliwa   uteuzi wao yeye kama  mbunge anaona  walichokipata  mawaziri hao ni haki yao  na kamwe hataacha  kuwapigania  wananchi  wake wa  Ludewa kwa  kuwanyoshea  vidole  mawaziri  wasiowajibika  katika nafasi  zao.

Kwani  alisema mbali  ya  mawaziri hao  bado  wapo  viongozi mbali mbali  wa  serikali ambao  wamekuwa  wakifanya kazi kimazoea kwa kushindwa  kuwajibika katika nafasi  zao na  kusababisha kero  kwa  wananchi na hata kuichukia  serikali yao   iliyopo madarakani.

Pia   alimpongeza  Rais Dr  Jakaya  Kikwete  kwa kutimiza  kwa wakati ahadi yake  ya gari la  wagonjwa katika Hospital ya wilaya ya  Ludewa ahadi ambayo aliitoa  wakati  wa  ziara  yake  mkoani Njombe  mapema mwaka  huu.

Kwani alisema  kuwa  utekelezaji wa ahadi za Rais  kwa  wananchi  wa  jimbo la   Ludewa  zinaendelea  kuwavutia  wananchi  wa  jimbo  hilo  na  kuwataka  wananchi  wa Ludewa  kuwa  wavimilivu  na kuendelea  kuwa na imani  na  viongozi  wao na  kuacha   kulalamika  pale  ahadi  husika  inapochelewa kutolewa .

Miongoni  wa   misaada  iliyotolewa  na  mbunge  huyo ni pamoja na marumaru seti 100, mifuko  20  ya  saruji  ,kinada  cha  kisasa kwa  ajili ya kanisa na  sare  seti  mbili  za kwaya  kanisani  hapo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE

JINSI BINTI HUYU MWANAFUNZI ANAVYOIPENDA MITI