Msichana mwenye umri wa miaka 14 kutoka Kenya amepata umaarufu duniani kwa jitihada zake za kuokoa sayari, kukutana na watu kama Mfalme Charles na kuungana na mshindi wa tuzo ya Grammy Meji Alabi na nyota wa zamani wa soka David Beckham katika kampeni dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi . Ellyanne Wanjiku Chlystun alikuwa na umri wa miaka minne pekee alipochochewa kuchukua hatua kuhusu suala hilo huku msukumo wake ukitoka kwa mpanda miti maarufu nchini Kenya na mshindi wa Tuzo ya Nobel, Prof Wangari Maathai. "Nilikuwa nikifanya mradi katika shule ya chekechea kuhusu watu ambao wamefanya mabadiliko duniani, kama vile Martin Luther King, Nelson Mandela na Florence Nightingale. "Hata hivyo, ni Wangari Maathai, mwanamke huyu wa ajabu wa Kenya, ambaye alikuwa amepanda mamilioni ya miti katika jamii yake ili kueneza ufahamu kuhusu upandaji miti , na jinsi gani unaweza kuendeleza nchi au bara, ambaye alinitia moyo," Ellyanne anaiambia BBC. Prof Maathai alitetea maoni kwamba wanaw
Comments