WASEMAVYO WANA KALENGA JUU YA KIFO CHA DR MGIMWA

Bw  Mario  Kihongo  katibu  uchumi  ,mipango  na  fedha  (CCM) kata ya Maboga

Mheshimiwa  Mbunge Dr  Wiliam Mgimwa  enzi  za  uhai  wake  alikuwa karibu  sana na  wananchi na hata maisha aliyopata  kuishi  ni tofauti na viongozi  wengine  katika   serikali  hii ya rais Jakaya  Kikwete.

"Natambua ni mapenzi  ya  Mungu  ila kweli  tulimpenda  sana mbunge  wetu  alikuwa ni mtu  wa  kujishusha asiyependa kujilimbikizia mali  zaidi ya  kuwatumikia  wananchi ....kweli  kifo  chake ni  pigo kubwa na hatujui  kama tutakuja  kumpata kiongozi anayefanana na Dr Mgimwa  katika  jimbo la kalenga"

Alikuwa ni  kiongozi  wa kushirikiana  vema na  wananchi  wake  katika  shida na raha  mfano kata  yetu  ya  Maboga  mheshimiwa Dr Mgimwa ametusaidia mnala wa simu kata ya Maboga  na alikuwa si wa  kujisikia  kweli  kifo  chake  kimetugusa  sana  kweli hatuna la kusema ni  Mungu ndie anajua .

Hata  hivyo  alisema ni  pengo  kubwa ambalo  wamelipata na hadi  sasa hawajui ni nani  wa  kuliziba  pengo  hilo na jimbo  hilo la kalenga  limepata  kuwa na wabunge  zaidi ya  watatu ila ni  yeye  pekee ndie  aliyepata  kutengeneza  miundo  mbinu katika maeneo mengi ya  jimbo.

Katika  uadilifu kweli  ushahidi  upo  wazi kutokana na mazingira ya nyumbani kwake Magunga  ambapo nyumba yake  ni ya kawaida  sana ukilinganisha na nyumba za wananchi wa kawaida na ni vigumu kuamini kama hapa ndipo nyumbani kwa  waziri wa fedha ama mbunge kwani alikuwa mwadilifu kama hayati  baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa  kuwajali  wananchi kwanza  kuliko yeye na familia  yake.
Dismas  Mbwela  binam  wa  Dr  Mgimwa
....................................................................................................................
Dr  Mgimwa alikuwa ni mtu  wa maendeleo na alikuwa habagui  na kitu akisema alikuwa akikitekeleza na  pale  inaposhindikana alikuwa akirudi na kutueleza  ukweli  kuwa imeshindikana na kutoa  sababu  za  kushindikana  tofauti na viongozi  wengine  ambao  hupenda  kusema uongo hata  pale  inaposhindikana kutimiza ahadi  zao 

Kweli  katika  familia  yetu  alikuwa ni mlezi  wa kweli  asiyembagua  mtu  na siku  zote  alikuwa ni mshauri wa familia  na  hata akirejea  kutoka bungeni  alikuwa akiishi  kijijini  tofauti na wabunge  wengine ambao  wamekuwa  wakiishi  mbali na  wapiga  kura   wao.
Bw  Martine  Simangwa  aliyekuwa katibu  wa  mbunge  Dr Wiliam Mgimwa .
 ...............................................................
 Aliyekuwa katibu  wa mbunge Dr Mgimwa Martine  Simangwa alisema  kuwa katika  uhai  wake mbunge  huyo alikuwa akitaraji  kuanza  kutimiza ahadi zake ambazo alipata  kuwaahidi  wananchi  hasa  ile ya  kusambaza mabati  katika  shule za  msingi na  sekondari.
 
Simangwa  alisema  walitegemea  kugawa  bati  zaidi  ya 1170  katika  shule  na idara ya afya na  kuwa bati hizo  alipanga  kuzifanya  ndani ya  wiki mbili  zijazo  na  siku  zote  alisisitiza  kuwa lazima atimizi ahadi  hiyo ya  mabati .

" Mimi kama  katibu  wake na niliyefanya nae kazi kwa karibu  zaidi  nitaendelea  kukumbatia urithi pekee alioniachia  mimi na  wana Kalenga   ambapo mara kwa mara  alisema kuwa ili nchi na  wananchi  waweze  kusonga mbele  katika uchumi ni lazima  kupata  elimu  bora na kujiendeleza kwa  elimu "

Alisema  kuwa moja kati  ya mambo ambayo alijipanga  kuyamalizia  kutekeleza kabla ya mwakani wakati  wa uchaguzi  mkuu ni pamoja na kuendelea  kumalizia  viporo  vya ahadi  zake  katika  sekta ya elimu, afya , miundo  mbinu na baadhi ya maeneo kutatua  kero  ya maji na kila  wakati hata  akiwa  Afrika ya kusini katika matibabu pindi wanapofanya mawasiliano  alikuwa ni mtu mwenye kupenda  kurejea ili  kuendelea na ziara ya  kutekeleza ahadi  zake kwa wananchi  wa  jimbo la Kalenga.



TANZIA
WAKUU WA IDARA/VITENGO
WATUMISHI WOTE
WIZARA YA FEDHA

TUNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA WAZIRI WA FEDHA MHE. DKT. WILLIAM A. MGIMWA (MB) KILICHOTOKEA TAREHE 01 JANUARI, 2014 HUKO AFRIKA KUSINI, KATIKA HOSPITALI YA KLOOF MEDI – CLINIC, PRETORIA.  MWILI WA MAREHEMU UNATARAJIA KUWASILI SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 04/01/2014 NA UTASAFIRISHWA KWENDA MKOANI IRINGA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 05/01/2014 KWA MAZISHI.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU
MAHALI PEMA PEPONI.  AMEN

2 JANUARI, 2014


OFISI YA WAZIRI MKUU
RATIBA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA
DKT. WILLIAM A. MGIMWA
TAREHE
SIKU
MUDA
TUKIO
WAHUSIKA
4.1.2014
JUMAMOSI
7.00 MCHANA
MWILI WA MAREHEMU KUWASILI UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE – TERMINAL II NA KUPELEKWA NYUMBANI MIKOCHENI B
NDUGU
VIONGOZI
WANANCHI
KAMATI
11.00 JIONI
MWILI KUPELEKWA HOSPITALI YA LUGALO
KAMATI
5.1.2014
JUMAPILI
3.00 – 4.00 ASUBUHI
CHAKULA NYUMBANI KWA MAREHEMU
KAMATI
4.30 ASUBUHI
MWILI KUWASILI NYUMBANI
KAMATI
5.30 – 8.00 MCHANA
MWILI KUPELEKWA UKUMBI WA KARIMJEE, KWA AJILI YA IBADA NA HESHIMA ZA MWISHO
KAMATI
8.00 MCHANA
MWILI KUPELEKWA UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE – TERMINAL 1
KAMATI YA KI - TAIFA
10.00 JIONI
MWILI KUWASILI IRINGA
(NDULI AIRPORT) NA KUAGWA KATIKA UKUMBI WA SIASA NI KILIMO - IRINGA
MKUU WA MKOA
KAMATI YA MKOA
KAMATI YA KI - TAIFA
11.30 JIONI
KUELEKEA KIJIJINI MAGUNGA
MKUU WA MKOA
KAMATI YA MKOA
KAMATI YA KI - TAIFA
6.1.2014
JUMATATU
6.00 MCHANA
SHUGHULI ZA MAZISHI KIJIJINI KWA MAREHEMU MAGUNGA
MKUU WA MKOA
KAMATI YA MKOA
KAMATI YA KI - TAIFA

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAMBO YANAYOUA NDOA NA MAHUSIANO

RAIS SAMIA ANA KWA ANA NA ZUHURA YUNUS

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

JINSI YA KUMSAHAU EX WAKO ALIEKUACHA;

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

USHAURI WA BURE KWA KILA MFANYAKAZI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE

JINSI BINTI HUYU MWANAFUNZI ANAVYOIPENDA MITI